Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania CTI Bw Leodger Tenga akizungmza leo Juni 13, 2023, kuhusu Maonesho ya Kimataifa ya wenye Viwanda Tanzania 2023 yanayotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
……………………………..
Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya wenye Viwanda Tanzania yajulikanyo kwa jina la Tanzania International Manufacturers Expo 2023 (TIME 2023) yatafanyika kuanzia Oktoba 4 mpaka 6 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Maonesho hayo yameandaliwa kwa ushirikiano baina ya Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE).
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania CTI Bw Leodger Tenga amesema Maonesho ya Kimataifa ya wenye Viwanda Tanzania 2023 yanaashiria hatua kubwa ya maendeleo ambayo sekta ya viwanda na biashara imepiga nchini.
Amesema lengo kubwa la maonesho haya ni kuunganisha sekta ya viwanda nchini na wenzao kutoka nje ya nchi kwa kutumia jukwaa moja ambayo yanatarajia kushirikikisha wazalishaji wa bidhaa za viwandani zaidi ya 500.
Mbali ya maonyesho haya, tukio hili pia litatamatisha Tuzo za Rais wa 17 za Wazalishaji Bora wa Mwaka (PMAYA). Ameongeza kuwa shughuli mbalimbali kama vile maonesho, utayarishaji wa mikutano (B2B), semina, mijadala na hotuba mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara maarufu wa Tanzania na nje ya nchi zitatolewa.
Mada mbalimbali katika tukio hili zitajadiliwa katika maonesho hayo kwa lengo la kutumia sera za hivi karibuni za maendeleo ya uchumi zinazosaidia ukuaji wa viwanda nchini Tanzania.
Maonesho hayo pia yatatambulisha mifumo mipya ya biashara na teknolojia ya kisasa ili kuleta mafanikio makubwa katika sekta husika katika tukio hilo ambapo CTI na TANTRADE wanatazamia kulifanya kila mwaka.
“Maonesho haya yatakuwa yatafanyika kwa kila mwaka na tunatarajia kuwa litakuwa jukwaa pekee la kufikia maendeleo katika sekta ya uzalishaji wa bidhaa za viwandani na kuweza kupata soko nje ya nchi kwa kupitia muunganiko maalum ambao utatokana na maonesho haya,” alisema Bw. Leodegar Tenga, Mkurugenzi Mtendaji wa CTI
Maonesho ya Kimataifa ya Wazalishaji Tanzania 2023 (TIME 2023) yataziba pengo kati ya uwezo wa sekta ya viwanda vya ndani na waagizaji, na wanunuzi wa bidhaa wa kimataifa.
Alisema kuwa katika siku zote tatu, watakaohudhuria watapata maarifa kuhusu mada zifuatazo: Utengenezaji wa Uchimbaji (metali, madini na plastiki) , Usindikaji wa Kilimo , Utengenezaji wa bidhaa zinazotumiwa na watumiaji , Kemikali za petroli , Madawa , Teknolojia ya nishati mbadala , Vifaa vya umeme , Vifaa na mitambo ya kisasa ya viwanda.
Aidha, Bw. Tenga amesema “Maonesho ya TIMEXPO 2023 yanatarajia kuwakutanisha pamoja Mawaziri, Washirika wa Maendeleo, Mabalozi na waanzilishi wa sekta binafsi na jumuiya ya kimataifa ili kujadili, kuunganisha na kutafuta fursa za ukuaji na mafanikio baina yao.”
“Tutatarajia uwepo wa wawakilishi wote wakuu wa sekta ili kuunda na kujenga tasnia ya utengenezaji,” aliongezea Bw. Leodegar Tenga.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Fortunatusa Mhambe amesema, “CTI na TANTRADE zimejipanga kujenga mazingira mazuri ya sekta ya viwanda nchini ili kuleta maendeleo makubwa kupitia maonyesho haya.”
Ni matarajio yetu kuwa TIMEXPO 2023 italeta mapinduzi makubwa katika sekta husika na kuleta mafanikio.
Tunaatarajia washiriki mbalimbali kutoka kona zote duniani. Tunatarajia kuwa na tasnia zetu maarufu za ndani kuonyesha bidhaa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Fortunatusa Mhambe akizungumza kwenye mkutano huo katikati ni Hussein Sufian Makamu Mwenyekiti CTI na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania CTI Bw Leodger Tenga
Hussein Sufian Makamu Mwenyekiti CTI akifafanua jambo katika mkutano huo kutoka kushoto ni Balozi wa Uganda nchini Tanzania Kanali Mstaafu Fred Mwesigye na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania CTI Bw Leodger Tenga.
Viongozi hao kwa pamoja wakiangalia makala fupi ya luninga wakati wauzinduzi huo.
Picha zikionesha wageni waalikwa mbalimbali walioshiriki katika mkutano huo.
John Mnali Mkurugenzi wa Uwekezaji na utangazaji Kituo cha Uwekezaji TIC akifuatilia mambo kadhaa katika mkutano huo.