Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe.Jaffar Haniu ameongoza zoezi la Kukabidhi wa pikipiki kwa Watendaji wa kata 06 na Maafisa Ugani 40 katika Halmashauri ya Busokelo Wilayani Rungwe zikiwa ni jitihada za Serikali katika kuongeza uzalishaji Mali Shambani ,kukusanya mapato sambamba na uimarishaji wa utawala bora. Akikabidhi pikipiki hizo, Mhe. Haniu ameagiza Watendaji hao wa Serikali kuhakikisha wanazitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuwaletea Maendeleo wananchi na kuwaondolea changamoto mbalimbali zinazowakabili hasa Vijijini. “
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe.Jaffar Haniu akizungumza wakati alipokabidhi pikipki kwa watendaji na maafisa ugani mbalimbali katika Halmashauri ya Busokelo Wilayani Rungwe zikiwa ni jitihada za Serikali katika kuongeza uzalishaji Mali Shambani.
…………………………….
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe.Jaffar Haniu ameshiriki Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe sambamba na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Akitoa salamu za Serikali katika baraza hilo, Mhe. Haniu ameishukuru Halmashauri hiyo kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa ufanisi na kuagiza Wakandarasi ambao hawajamaliza hiyo kufanya hivyo kwa wakati ili wananchi wapate huduma stahiki na Kwa wakati.
Wakati huohuo Mhe. Haniu ameaagiza Watalamu mbalimbali katika Halmashauri hiyo kukusanya mapato ya Serikali kwa bidii huku akiomba Madiwani kuendelea kumulika vyanzo vya mapato katika maeneo yao ili kusaidia kutekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Aidha ameliomba baraza hilo kusimamia kwa ukaribu utoaji wa mikopo ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu ikiwa ni asilimia kumi ya mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo.
Mhe.Haniu ameongeza kuwa mikopo hiyo hutolewa na Serikali ili kuinua kiwango Cha Pato kwa wananchi hivyo Halmashauri haina budi kutoa kwa wakati na kusimamia urejeshwaji wake ili iwanufaishe na wengine.
Katika hatua nyingine Mhe . Mhe Haniu ameeleza kuwa Serikali imekuwa ikihamasisha wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto wenye umri wa kujiunga na elimu ya Msingi sambamba na kidato Cha kwanza hivyo kila mzazi na jamii Kwa ujumla ina wajibu wa watoto wote wanaenda shule.
Halmashauri ya Busokelo mpaka sasa wanafunzi wa kidato cha kwanza wameripoti kwa asilimia 92% na darasa la kwanza asilimia 103%.
Aidha ameshukuru shule zote zinazotekeleza zoezi la chakula Cha mchana kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari na kuagiza wazazi wote ambao hawajaanza kutekeleza zoezi hilo kuanza kufanya hivyo ili kuondoa udumavu na utapiamlo kwa wanafunzi na kuongeza ufaulu shuleni.
Akizungumzia migogoro ya Ardhi, Mhe. Haniu amekea migogoro inayoendelea katika ngazi ya kaya na Jamii na kuwa utatuzi uendelee kwa kufuata taratibu zilizowekwa kwa kuwashirikisha viongozi, na Baraza la Ardhi.
“Migogoro mingi inatoka ngazi ya kaya ni vema suluhisho lake pia likaanzia ngazi ya kaya badala ya kugombana na kuhatarisha amani katika jamii” Amesisitiza Mhe.Haniu