Weisiku Chacha ambaye ni mhitimu na mnufaika wa mfuko huo katika Manispaa ya musoma akizungumza na waandishi wa habari waliomtembelea katika biashara yake ya matunda mtaa wa Mkinyerero kata ya Mwisenge mjini Musoma.
Weisiku Chacha ambaye ni mhitimu na mnufaika wa mfuko huo katika Manispaa ya musoma akimhudumia mmoja wa wateja wake waliofika kwenye genge lake ili kununua mahitaji yao.
Raia wa Kigeni pia hufika katika eneno la baishara ya Weisiku Chacha na wenake kwa ajili ya kupata mahitaji wamatunda na mbogamboga.
………………………………………..
Wananachi 904 kutoka mitaa 39 katika ya mitaa 71 ambao ni manufaika wa TASAF waliokuwa wakihudumiwa katika mpango wa TASAF wa kunusuru kaya masikini Kwa muda wa miaka 8 wanaondoka kwenye mfumo wa huduma hiyo katika manispaa ya Musoma baada ya uchumi wao Kuimarika na Sasa wanaendelea na Biashara zao ndogondogo
Hayo yamelezwa Leo na Mratibu wa TASAF Manispaa ya Musoma Bw Octavian Rweyemamu wakati alipozungunza Katika ziara ya maafisa Kutoka TASAF Makao Makuu mkoani Dodoma ambao waliwatembelea wahitimu hao Kwa lengo la kuona shughuli za mafanikio Kwa kipindi walichokuwa wakihudumiwa na mpango huo wa TASAF.
Kwa upande wake Ofisa Habari wa TASAF Kutoka Makao Makuu Bw. Christopher Kidanka amewapongeza wanufaika hao kwakuwa wameonyesha bidii kubwa ya kuzitumia vyema pesa hizo kwa kuanzisha Biashara zao ndogo ndogo ambazo zimeweza kuwakwamua katika janga la umaskini.
“Sisi kwetu kama TASAF tunawaona nyinyi kama mashujaa kuna watu wanafanya kazi kubwa na nzuri tu lakini hadi anastaafu hana hata nyumba lakini nyie kwa sasa mmefanikiwa na mnajimudu kimaisha kwa kiasi fulan,” Amesema Kidanka.
Ameongeza kwamba watachukua wanufaika wachache wanaondoka kwenye mpango huo na wataenda kutembelea miradi yao ili kujionea na kuonyesha kwa wananchi wengine jinsi wanufaika hao walivyoweza kuitengeneza na kuendeleza miradi ya kupitia hela za Mfuko wa TASAF.
Kwa Upande wake Weisiku Chacha ambaye ni mhitimu na mnufaika wa mfuko huo katika Manispaa ya musoma amesema anashukuru mfuko huo kumkwamua kwenye Janga la umaskini kwani kipindi cha nyuma alikuwa na maisha magumu ila kwa sasa hivi watoto wangu wanasoma vizuri na wanakula milo mitatu.
“Nilipoanza na hela ya TASAF nilifungua kibanda cha matunda baada ya mwaka mmoja nikanunua ng’ombe watatu na mbuzi wawili na bado naendelea na Biashara ya matunda inaendelea kunipatia kipato na endapo ikitokea nikaondolewa kwenye mfuko huo ninauwezo wa kuendelea kusimamia Biashara, mifugo na nikajikimu kimaisha mimi na familia yangu,’
Amesema Weisiku Chacha.
Aidha Weisiku ametumia fursa hiyo kuwashauri wananchi ambao wataingizwa kwenye mfuko huo kwa sasa kuzitumia vizuri fedha watakazopewa kuziwekeza kwenye Biashara ndogo ndogo ili ziweze kuwakwamua katika Janga la umaskini.