Mratibu Taifa Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu nchini THRDC Onesmo Ole Ngurumwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mfumo jumuishi wa kidigitali wa utoaji huduma za utetezi wa haki za binadamu ambao wameupa jina la Watetezi Data Base iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.Mtaalamu wa mfumo wa huduma jumuishi kwa wanachama wa mtandao huo,ambaye ni Mkurugenzi wa Bluefin Solution Limited Mussa Kisena akiuelezea mfumo jumuishi wa kidigitali wa utoaji huduma za utetezi wa haki za binadamu ambao wameupa jina la Watetezi Data Base iliyofanyika leo jijini Dar es salaamMkuu wa Dawati la Wanachama wa Mtandao huo Lissa Kagaruki akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mfumo jumuishi wa kidigitali wa utoaji huduma za utetezi wa haki za binadamu ambao wameupa jina la Watetezi Data Base iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
……………………..
NA MUSSA KHALID
Imeelezwa kuwa upatikanaji duni wa taarifa katika mifumo ya utetezi wa haki za binadamu umetajwa kurudisha nyuma juhudi za utetezi wa haki za binadamu nchini.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mratibu Taifa Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu nchini THRDC Onesmo Ole Ngurumwa katika hafla ya uzinduzi wa mfumo jumuishi wa kidigitali wa utoaji huduma za utetezi wa haki za binadamu ambao wameupa jina la Watetezi Data Base.
Mratibu wa THRDC Olengurumwa amesema mfumo huo utarahisisha upatikanaji wa taarifa kwa mashirika wanachama zaidi ya 200 ya mtandao huo nchini.
Aidha Olengurumwa amesema urahisi katika upatikanaji taarifa utaboresha hali ya haki za binadamu nchini kutokana na taarifa zihusuzo haki za binadamu kupatikana kwa urahisi..
‘Katika Dunia ya sasa hivi tunaondokana na shughuli za makaratasi ili kuweza kuokoa muda hivyo tumeamua kuzindua website mpya ambayo itakwenda sambamba na mfumo huo wa usajili ufuatiliaji na usimamizi wa wanachama wetu’amesema Mratibu Olengurumwa
Amesema kuwa mategemeo yao wanachama wote wataanza kuutumia rasmi mfumo huo baada ya kufanyika kwa uzinduzi wa leo jambo ambalo litakalosaidia kufanikisha huduma za utetezi kwa haraka.
Katika hatua nyingine mtaalamu wa mfumo wa huduma jumuishi kwa wanachama wa mtandao huo Mussa Kisena amesema huduma jumuishi kwa mashirika wanachama wa mtandao huo utarahisisha shughuli za mtandao huo ikwemo ujengaji uwezo kwa wanachama wa mtandao huo
‘Katika mfumo huu tumezingatia mazingira yenye kiwango kikubwa cha usalama wa kimataifa hivyo hakuna namna yeyote wadukuzi wa kimtandao wanaweza kuingilia na kupata taarifa isivyo halali’amesema Kisena
Kwa upande wake Hata hivyo Mkuu wa Dawati la Wanachama wa Mtandao huo Lissa Kagaruki amewasihi wanawake watetezi wa haki za binadamu nchini sambamba na changamoto wanazokumbana nazo katika utetezi kuendelea na juhudi hizo.