Home Mchanganyiko WAZIRI BALOZI DKT. CHANA ASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA FAO.

WAZIRI BALOZI DKT. CHANA ASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA FAO.

0

…………………..

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameshiriki Mkutano wa Kimataifa chini ya Shirika la Chakula Duniani ( FAO) ulioendeshwa kwa njia ya mtandao kujadili masuala ya uzalishaji chakula na misitu.

Akishiriki mkutano huo uliokuwa na wadau zaidi ya 1500 kutoka nchi mbalimbali jijini Dodoma, Waziri Balozi Dkt. Chana amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka Sera nzuri zinazoishirikisha jamii katika uhifadhi wa Misitu.

Waziri Balozi Dkt. Chana ameeleza kuwa kupitia mifumo mizuri, Sera na Sheria juu ya Usimamizi na Matumizi endelevu ya Rasilimali ya Misitu nchini jamii inashiriki kikamilifu katika uhifadhi wa rasilimali hiyo kwa maslai mapana ya Jamii na Taifa kwa Ujumla.

Katika mkutano huo Tanzania imeshiriki kama mjumbe ambapo Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Chana amewasilisha mada Juu ya Mifumo ya Sera na Sheria ya Usimamizi na Matumizi Endelevu ya Rasilimali ya Misitu Tanzania.

Mkutano huo umefunguliwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Divisheni ya Misitu FAO Bi.Tiina Vahanen akiwa nchini Itali na kuhudhuriwa pia na Mwakikishi wa Mkurugenzi wa Misitu, Bw James Nshare na Afisa Misitu Mwandamizi Bw.John Wanjala.