Home Mchanganyiko WATENDAJI WA DAWATI LA LINSIA NA WATOTO MKOA WA SINGIDA WAPATIWA MAFUNZO

WATENDAJI WA DAWATI LA LINSIA NA WATOTO MKOA WA SINGIDA WAPATIWA MAFUNZO

0

Na A/INSP FRANK LUKWARO

Watendaji wa Madawati ya Jinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi wametakiwa kujikita katika kutoa elimu kwa Wananchi ili kukabiliana na Vitendo vya Ukatili nchini kwa kuwa kila Mwananchi akiapata elimu itasaidia kupunguza vitendo hivyo.

Hayo yamesemwa leo mkoani Kilimanjaro na Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto, Naibu Kamishna wa Polisi Maria Nzuki wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa Watendaji wa Dawati hilo kutoka mkoa wa Singida yanayofanyika Shule ya Polisi Tanzania zamani CCP kwa lengo la kuwajengea uwezo kukabiliana na Makosa ya Ukatili wa Kijinsia na Unyanyasaji wa Watoto.

Kwa Upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi Stella Mutabihirwa amesema mafunzo hayo yatawafikia Wadau wote akiwemo watendaji wa Kata na Mitaa ili kuzuia makosa ya ukatili.

Naye Mratibu wa Mradi wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia kutoka Shirika la UN WOMEN Bi. Lucy Tesha amesema wanatarajia kujenga ofisi za Dawati la Jinsia na Watoto katika  Wilaya za Ikungi na Mkalama kutokana na Wilaya hizo kuwa na idadi kubwa ya matukio ya Unyanyasaji wa Kijinsia katika mkoa wa Singida.