Nelly Kisanga Mkurugenzi wa vipindi wa Wasafi Media akizungumza leo kwenye hoteli ya Serena wakati walipotambulisha kampeni mpya ya “Chota Mihela” ambayo wananchi mbalimbali wataweza kujishindia kwa kusikiliza vipindi mbalimbali vya redia hiyo katika uzinduzi uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mtangazaji Lil Ommy akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo uiofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Picha zikionesha baadhi ya watangazaji wa Wasafi Media wakiwa katika uzinduzi huo.
UONGOZI wa Wasafi Media wameitambulisha rasmi Kampeni ya Mchezo wa ubashiri inayokwenda Kwa jina la “Chota Mihela” kama sehemu ya kugawa pesa Kwa wasikilizaji na watazamaji wa wasafi.
Akizungumza mara baada kutambulisha Kampeni hiyo Mkuu wa Kitengo cha Ubunifu Cha Wasafi Media Lily Ommy amesema Kampeni hiyo imekidhi vigezo na imepewa dhamana na bodi ya Michezo ya ubashiri Huku watu chini ya Miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki na atakaeibuka Mshindi pesa zake atatumiwa kwenye namba aliyoitumia kutupia ubashiri wake.
“Vipindi vyote kutoka wasafi tv na wasafi redio vitakua vinatoa pesa kupitia Kampeni ya “Chota mihela” Kwa Kila siku na Kila lisaa milioni 1 Kwa washindi 10 na milioni 5 Kwa Mshindi 1.”
Kwa upande wake Mtangazaji wa kipindi cha ‘Masham sham’ katika redio ya wasafi fm Khadija Shaibu maarufu kama ‘Dida Shaibu’ amesema Kampeni hiyo
itaenda kusaidia wamama Wenye uhitaji hasa Wafanyabiashara wadogo wadogo hususani wamama ntilie ,wauza vitumbua kupitia Kampeni hii inaenda kukupa mtaji wa kibiashara kwani Kipindi cha Masham sham kimekua msaada wa kutoa mitaji Kwa wakina mama hivyo itakua msaada sana Kwenye hilo.
Hata hivyo Kampeni hiyo mara baada ya kutambulishwa wasikilizaji walipewa nafasi ya kufanya ubashiri wao katika kuizindua Kampeni ya “Chota Mihela”
na hatimae Msikilizaji kutoka Mkoa wa Kilimanjaro Prince Heri Mwanga akaibuka Mshindi wa shilingi milioni 5 .