Home Mchanganyiko DK. PHILIP MPANGO: TANZANIA INAUNGA MKONO NA KUAMINI TAFITI KATIKA KUKABILIANA NA...

DK. PHILIP MPANGO: TANZANIA INAUNGA MKONO NA KUAMINI TAFITI KATIKA KUKABILIANA NA MARADHI

0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na washiriki wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 31 wa pamoja wa Sayansi ulioandaliwa na  Taasisi ya Taifa ya utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) unaofanyika katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akitoa tuzo za Sayansi kwa washindi mbalimbali  wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 31 wa pamoja wa Sayansi ulioandaliwa na  Taasisi ya Taifa ya utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) unaofanyika katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

Washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango wakati akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 31 wa pamoja wa Sayansi ulioandaliwa na Taasisi ya Taifa ya utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) unaofanyika katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es salaam. leo tarehe 17 Mei 2022.

Picha ya pamoja.

Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari Kando ya Mkutano huo mara baada ya kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango.

Robeta Feruz Afisa Mwasiliano na Elimu Kwa Umma (TMDA) akitoa maelezo kwa baadhi ya wanasayansi waliotembelea banda la (TMDA) katika maonesho yanayofanyika kando ya mkutano huo.

Majadiliano Kidogo

Maltin Malima Afisa Uhusiano Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA)  akizungumza na mmoja wa wataalam wa tafiti za  kisayansi waliotembelea katika banda la (TMDA).

Sigifrid Mtei Afisa Uelimishaji Umma ITMDA) wakitoa elimu kwa wataalam mbalimbali waliotembelea  kwenye banda la Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA).

Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Bi. Gaudensia Simwanza kushoto na Robeta Feruz Afisa Mwasiliano na Elimu Kwa Umma TMDA wakiwa katika mkutano huo.

Baadhi ya wataalamu kutoka NIMR wakiwa na vifaa vyao vya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ikiwemo kifua kikuu wakiwa kwenye maonesho yanayofanyika kando ya mkutano huo wa siku tatu.

………………………………..

 Tanzania inaunga mkono na kuamini katika kufanya tafiti zitakazokabiliana na changamoto za maradhi hapa nchini kwa sababu tafiti ndizo zinaweza kusaidia kutambua changamoto mbalimbali za kiafya zinazomkakabili binadamu.

 Mkutano huu ni fursa ya aina yake kwa wanasayansi wa Tanzania kujifunza kutoka kwa kila mmoja na kuunganisha werevu na uwezo wao katika kupata masuluhisho ya kimsingi kwa changamoto kuu za kiafya hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango  leo Mei 17,  2022 wakati akifungua mkutano wa 31 wa pamoja wa wanasayansi ulioandaliwa na Taasisi ya Taifa ya utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na kufanyika kwenye kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

Dk. Mpango ametanabaisha kuwa mkutano huo una umuhimu mkubwa kutokana na kufanyika katika kipindi ambacho dunia, Tanzania ikiwemo inapitia katika changamoto mbalimbali za magonjwa kama vile Uviko 19 pamoja na magonjwa yasioambukiza. Aidha ameongeza kwamba serikali imedhamiria kufikisha huduma za kiafya katika maeneo yote hapa nchini na itaendelea kushirikiana na wadau wote wakiwemo watafiti na sekta binafsi.

Aidha Makamu wa Rais ameiagiza Taasisi ya Taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR) kuongeza kasi ya ufanyaji utafiti pamoja na kuzalisha chanjo na dawa bora za asili.

Kwa upande wake Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema wizara itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa Taasisi ya Taifa ya utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ili kuweza kutumiza majukumu yao kwa ufanisi.

Amesema tayari NIMR imeshiriki katika tafiti mbalimbali zinazowezesha katika utungaji wa sera na mipango katika wizara ya afya ikiwemo kuwezesha Wizara kupata uhalisia wa utoaji wa chanjo ya HPV ambayo inakinga wasichana dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi.

Aidha, Waziri Ummy amewaagiza NIMR kuangalia namna ya kupanda mashamba pori kwa ajili ya dawa za Asili.

“Tumeona wakati wa wimbi la Ugonjwa wa Corona, dawa za asili zilisaidia sana wananchi.

Hivyo NIMR iangalie sehemu kama kule Mkoa wa Kagera Mkoa wa Tanga, angalau wakapaga hata mashamba kadhaa ya kulima majani na miti ya madawa asili” Alisema” Waziri Ummy.

Aidha, aliwapongeza washindi wanne, walioshinda ambapo amewataka wakawe mfano katika utafiti.

Mkutano huo unashirikisha wataalamu na wadau mbalimbali wa sekta ya afya kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.