Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania TMA imetoa utabiri wake ambapo imesema kunatarajiwa kunyesha mvua kubwa katika maeneo machache ya mikoa ya Singida, Dodoma, Morogoro, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Ruvuma Lindi na Mtwara.
Meneja wa Kituo Kikuu cha Utabiri wa haliya hewa Bw.Samwel Mbuya akitangaza taarifa ya utabiri huo ametoa angalizo kuwa kuanzia Jumamosi Februari 5, 2022 mpaka Jumanne Februari 8,2022 wakati alipotangaza utabiri huo makao makuu ya mamlaka hiyo jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam leo.
Aidha metoa angalizo la kuwepo kwa upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.0 ikihusisha baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya kusini ya bahari ya Hindi (mikoa ya Lindi na Mtwara.
Mbuya pia ametoa angalizo kuwa kutakuwepo na upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa kwa baadhi ya maeneo ya ziwa Nyasa (mikoa ya Ruvuma, Njombe na Mbeya).
Ameongeza kuwa kutokana na hali hiyo upo uwezekano kutokea kwa baadhi ya makazi ya watu kujaa maji, pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za usafirishaji na uvuvi, Nyumba zenye mapaa yasiyoimara kuezuliwa, kuanguka kwa miti midogo na kukatika kwa matawi ya miti mikubwa.
Akizungumzia utabiri wa Jumapili 06-02-2022 ametoa angalizo kuwa kunatarajiwa mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dodoma, Morogoro, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Iringa, Njombe, Ruvuma Lindi na Mtwara.
Ameongeza kuwa upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.0 utakuwepo kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya kusini ya bahari ya Hindi (mikoa ya Lindi na Mtwara.
Amesema pia upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa utakuwepo kwa baadhi ya maeneo ya ziwa Nyasa (mikoa ya Ruvuma, Njombe na Mbeya).
Ametanabaisha kuwa athari zinazoweza kujitokeza kwa baadhi ya makazi ni kujaa maji, pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za usafirishaji na uvuvi, nyumba zenye mapaa yasiyoimara kuezuliwa, kuanguka kwa miti midogo na kukatika kwa matawi ya
miti mikubwa.