Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano Vodacom Tanzania PLC, Rosalynn Mworia ( wapili kushoto ) akichangia mada kwenye kongamano la siku ya mtoto njiti lililozungumzia marekebisho ya muda wa nyongeza wa likizo kwa wazazi ili kupata fursa ya kulea mtoto aliyezaliwa njiti. Kampuni hiyo kwa sasa inatoa likizo ya uzazi ya miezi minne kwa wazazi wote wawili pindi wanapopata mtoto.Wengine kushoto ni msimamizi wa wodi ya watoto wanaopata huduma ya Kangaroo Hospitali ya Muhimbili , Sista. Cleopatra Mtei, mama shuhuda aliyejifungua mtoto njiti, Nikita Mandan na kulia ni muongoza mada, Innocent Mungy.