Na Silvia Mchuruza
                                     Bukoba,Kagera.

Zao la kahawa aina ya Robusta lmetajwa kuongeza tija na uzalishaji  mkoani Kagera  kupitia kwa wakulima wadogo wadogo licha ya kuwepo changamoto mbalimbali hasa changamoto ya kifedha 

Kauli hiyo imetolewa na afisa biashara wa mkoa wa Kagera Ndg. Issaya Tendega  aliekuwa mgeni rasmi  katika kikao kilichowahusisha wadau wa zao la  kahawa kupitia mradi wa Cafe Africa  kilichofanyika katika ukumbi wa ELCT HOTEL BUKOBA kwa niaba ya katibu tawala ma mkoa.
Tendega amesema Licha ya kuongezeka kwa uzalishaji wenye tija kubwa katika zao la kahawa bado changamoto zipo hasa katika suala la kifedha na masoko.
Nae mkurugenzi wa Cafe Africa Bi. Dafrosa  Sanga. amesema kuwa kahawa aina ya Robusta imeongezeka  katika uzalishaji licha ya kuwepo vitendo vya Butura na mikahawa ya zamani  kuwa mizee tayari ambapo mradi huu umefanya jitihada za kuchipusha tena mikahawa hiyo.
Aidha amesema kuwa Cafe Africa ni mradi wenye lengo la kuinua zao la kahawa kuliongezea thamani na tija kwa wakulima katika uzalishaji ambapo mradi huo ulikuwa na lengo la kuwafikia wakulima wa wilaya zote za mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na vyama vikuu  vya ushirika KCU na KDCU.
Hata hivyo ameongeza kuwa vyama vya msingi vikubwa na vidogo  vilivyolengwa kufikiwa ni 250 na wakulima 22250 ambapo pia mradi  umetoa mafunzo kwa maafisa ugani 445, mpaka Sasa wamefikiwa wakulima 16384 na maafisa ugani 320 na kufanikiwa kuanzisha mashamba darasa 207.  
Pia Bi. Dafrosa ameongeza kwa kusema mradi umeendelea kuboresha miundombinu  kwa kushirikiana na wadau  wa zao la kahawa ambapo tayari mradi umechipusha miti laki sita (600,000) na kukarabati vitaru 4 katika wilaya 4 kikiwemo kitaru Cha Maruku ili kuwainua wakulima  katika uchumi wao kufikia mwaka 2025.