Na Mwandishi wetu, 

Msimu wa Korosho 2026/2027 umezinduliwa rasmi na Emmanuel Shilatu kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Masasi ambapo amewataka viongozi wa Amcos kutokuichezea ama kuihujumu Korosho maana wataishia kufungwa. 

Shilatu ameyasema hayo kwenye kikao Cha uzinduzi wa msimu wa Korosho 2026/2027 kilichohusisha Wadau mbalimbali wa Korosho.

” Wakulima wa Korosho wanamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoliheshimisha zao la Korosho. Serikali haitamvumilia Mtu yeyote atakayefanya mzaha ama kujaribu kuhujumu kazi nzuri iliyofanywa na Rais Samia kwa kutaka kuhujumu zao la Korosho kwa namna yeyote ile na hatua Kali zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo adhabu ya kufungwa. Alisema Shilatu.

Nae Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika wa Mkoa wa Mtwara Ndugu Robert Nsunza amewataka Makarani kutumia mizani ya kidigitali, kuzingatia ubora na kuwa Waadilifu.

Kiongozi wa chama kikuu Cha MAMCU Bi Biadia Matipa amesisitiza wamejipanga vilivyo na maandalizi yote yapo tayari na amehaidi kuhakikisha Wakulima kulipwa fedha zao mapema sana ndani ya siku 7 toka Mnada ufanyike.

Kwa upande wa viongozi wa Amcos wamehaidi uadilifu na utendaji kazi uliotukuka kwenye msimu huu wa Korosho 2026/2027.