Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Legal Services Facility Tanzania (LSF) Lulu Ng’wanakilala, akiwa kwenye picha ya pamoja na wazungumzaji na Baadhi ya watendaji wa LSF mara baada ya kumalizika kwa Mkutano huo.
Na: Hughes Dugilo, DODOMA.
Serikali imesesema kuwa inatambua na kuthamini mchango wa Asasi
za kiraia nchini katika kuchangia maendeleo ya nchi na uchumi wa mtu mmoja
mmoja kupitia utawala wa sheria na haki.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya uratibu wa Sera
Ofisi ya Rais TAMISEMI Enock Nyanda alipokuwa akiwasilisha mada kwenye mkutano
ulioandaliwa na Shirika la Legal Services Facility Tanzania (LSF) uliokuwa ukizungumzia
juu ya utawala wa sheria kuwa kichocheo cha kupunguza umasikini na kuleta usawa
wa kijinsia uliowakutanisha pamoja wadau
mbalimbali zikiwemo Asasi za kiraia ili kupata mawazo ya pamoja kwenye suala
zima la utawala wa sheria.
Amesema kuwa nguvu ya pamoja inaitajika kati ya
Serikali na Asasi za Kiraia katika kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuelewa umuhimu
na faida za utawala wa Sheria katika huduma mbalimbali za kijamii na Taifa kwa ujumla
“Kimsingi Ofisi ya Rais TAMISEMI ina jukumu kubwa
la kusimamia utawala wa Sheria na hii ina maana nyingi lakini inagusia suala
zima la makusanyo na matumizi ya fedha pia kusimamia suala la ulinzi na usalama
katika ngazi ya Serikali za mitaa ambazo ndizo nguzo kuu za uboreshaji wa
huduma za kijamii ambapo Ofisi ya Rais TAMISEMI imepewa jukumu hilo kusimamia Kikatiba
na Sheria” Amesema Nyanda.
Ameongeza kuwa
moja ya majukumu yao kama Wizara ni pamoja na kuratibu na kusimamia shughuli za
Asasi za Kiraia ili kujua Asasi ipi inafanya kitu gani na eneo gani ikiwa ni
sehemu ya kuchangia jitihada za Serikali katika kutatua changamoto zilizopo
katika jamii.
Naye katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji
Wanachi kiuchumi (NEEC) Beng’i Issa akijibu swali lililohoji ni namna gani
Serikali inachingia kuwainua vijana kiuchumi, ameeleza kuwa yapo maeneo mengi
ambayo Serikali imewawezesha vijana kukua kiuchumi ikiwemo elimu mbalimbali za
ujasiriamali na stadi za kazi zinazowawezesha kujiajiri wenyewe
“Tumetengeneza mwongozo wa kufundisha ujasiriamali
sasa unafundishwa kuanzia Shule za Msingi mpaka Vyuo Vikuu, hizi ni juhudi za Serikali
kuwasaidia vijana waweze kutumia elimu zao kujiajiri wenyewe
Akizungumza katika mahojiano maalumu mara baada
ya kumalizika kwa mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Legal Services
Facility Tanzania (LSF) Lulu Ng’wanakilala, amesema kuwa, Shirika lao mpaka
sasa limetoa msaada wa huduma za Kisheria kwa wananchi zaidi ya milioni 6 nchi
nzima ambao wamefikiwa moja kwa moja na watoa huduma za kisheria waliopo kwenye
mikoa yote Bara na Visiwani.
Ameongeza kuwa mafanikio makubwa ya watoa hutuma hao
wa kisheria yamefikia asilimia sabini na tatu (73%) ambao kesi zao
zimeshughulikiwa moja kwa moja na watoa huduma hao na kuzimaliza kabla ya
kufika kwenye ngazi za juu za sheria
“Kesi nyingi zinazokuja kwetu huwa zinasuluhishwa
hata kabla hazijafika kwenye vyombo vya juu na haya ni mafanikio makubwa hata
kwa Serikali kwani inapunguza mrundikano na msongamano wa kesi nyingi mahakamani
lakini pia hata zile gharama za uendeshaji wa kesi zinapungua sana, wanufaika
wakubwa ni wananchi wa kawaida kutokana na kutokuwa na uwezo wa kifedha”
Amesema Ng’wanakilala.
Aidha kutokana na umuhimu wa watoa huduma za
kisheria katika jamii (Paralegals) Asasi za kiraia zimechangia kuwezesha
Serikali kuwatambua rasmi kwa kutungiwa sheria inayowatambua kama chombo muhimu
cha kuifikia jamii kwenye ngazi ya chini.
Amesema, Shirika
lao limejikita kwenye upatikanaji wa haki wakiamini kuwa utawala wa sheria ni
kitu muhimu katika kuhakikisha wananchi wanapata haki zao za msingi