Mgeni rasmi na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya (mwenye suti nyeusi) akisikiliza maelezo ya juu ya utendaji kazi wa TMA kutoka kwa Mkurugenzi wa Tehama na Huduma za ufundi, Dr Pascal Waniha alipotembelea banda la TMA wakati wa Mkutano wa 14 wa sekta ya Uchukuzi wenye lengo la kupima utendaji wa sekta mbali mbali za uchukuzi alipotembelea banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Mtaalam wa Hali ya Hewa toka TMA, Abubakar Lungo (kushoto) akimweleza mgeni rasmi na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya (kulia) namna TMA inavyofanya kazi na wadau walioshiriki Mkutano wa 14 wa sekta ya Uchukuzi wenye lengo la kupima utendaji wa sekta mbalimbali za uchukuzi. Katikati ni Mkurugenzi wa Tehama na huduma za ufundi, Dr. Pascal Waniha akifuatilia
Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Tehama na huduma za ufundi, Dr. Pascal Waniha (kulia) kwenye Banda la TMA waliposhiriki Mkutano wa 14 wa sekta ya Uchukuzi uliokuwa na lengo la kupima utendaji wa sekta mbalimbali za uchukuzi.
…………………………………………
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema ni vyema ujenzi wa miradi yeyote hapa nchini kuhakikisha unafuata utaratibu wa kitaalamu wa hali ya hewa ili kufahamu mazingira ya hali ya hewa katika utekekezaji wa miradi ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kwa kutozingatia utabiri wa wataalam wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Mhandisi Kasekenya ameyasema hayo wakati jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwenye Mkutano wa 14 wa sekta ya Uchukuzi wenye lengo la kupima utendaji wa sekta mbalimbali za uchukuzi
Taasisi mbalimbali zinazotekeleza miradi nchini ni muhimu zikatumia sana taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa sababu hata utekelezaji wa miradi hiyo utakwenda kwa malengo yaliyokusudiwa, lakini pia ni rahisi kujua endapo kutatokea changamoto yoyote nchini kutokana na hali ya hewa ili ziweze kuchuhuku tahadhari kabla ya kutokea madhara.
Amesema TMA imesaidia sana sekta ya uchukuzi kwa kuendelea kutoa taarifa za Hali ya Hewa ambazo zinasaidia katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya usafirishaji wa ardhini na majini pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya kimaendeleo.
“Taasisi hii ni muhimu kwani inasaidia sekta zote katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati hususani ya barabara, Majini na kufahamu taarifa za hali ya hewa kwa yanayotarajiwa kutokea na kwa wakati gani,”. Amesema Kasekenya
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt Agness Kijazi amesema Mamlaka hiyo imekuwa ikitumika kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye sekta ya uchukuzi ikiwemo Anga,kwenye Reli,masuala ya barabara,na miradi mikubwa ya ujenzi hata bwawa la Nyerere ambalo linaendelea na ujenzi.
‘Sisi tupo hapa kuwaonyesha ni huduma gani tunazozitoa na kuwaonyesha jinsi tunatoa utabiri na namna unavyotumika kwani ni muhimu katika sekta hizo na hasa katika kipindi hiki ambacho kuna mabadiliko ya tabia ya nchi DUNIANI hivyo tunawaeleza wanavyoweza kuzitumia tabiri tunazozitoa katika shughuli zao’amesema Dkt Kijazi
Hata hivyo Dkt Kijazi ameziasa taasisi mbalimbali kuangalia masuala ya hali ya hewa ili kuepukana na kuweka mradi mikubwa kisha baadae likaja janga moja kubwa na kuufuta na kujikuta unanza upya.
Mkutao huo 14 wa sekta ya Uchukuzi umezishirikisha taasisi mbalimbali za kiserikali zikiwemo za usafirishaji wa Ardhini na Majini kwa malengo ya kujadili utendaji kazi wa taasisi hizo katika ufanyaji wa shughuli zao.