Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa tatu kulia), akizindua promesheni ya Bonge la Mpango awamu ya pili, ikiwa na lengo la kurejesha faida kwa wateja pamoja na kuhamasisha utamaduni wa kujiwekea akiba kwa Watanzania. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto), pamoja na maofisa waandamizi wa benki hiyo wakizindua rasmi promesheni ya Bonge la Mpango awamu ya pili. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Miongoni mwa zawadi ya toyo yenye thamani ya shilingi milioni 4.4 ikioneshwa kwenye uzinduzi huo. Jumla ya zawadi za toyo 50 kila moja ikiwa na thamani ya shilingi milioni 4.4 zitatolewa kwawashindi awamu hii.
Sehemu ya magari ya matangazo ya promesheni ya Bonge la Mpango awamu ya pili, yakinogesha uzinduzi wakati wa hafla hiyo.
………………………………………….
Benki ya NMB imezindua promosheni kubwa kabisa itakayoiunganisha benki hiyo na wateja wake pamoja na wateja wapya.
Promosheni hiyo inaitwa Bonge la Mpango Awamu ya pili.
Bonge la Mpango Awamu ya pili inakusudia kurejesha faida kwa wateja pamoja na kuhamasisha utamaduni wa kujiwekea akiba kwa Watanzania na hii ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Bonge la Mpango iliyozinduliwa mwezi Februari.
Leo tunakuja na Bonge la Mpango awamu ya pili.
Kampeni hii itawawezesha wateja kushinda fedha taslimu na pikipiki za miguu mitatu maarufu kwa jina la Toyo kama mtakavyoshuhudia muda wakati tukiizindua.
Kama mnakumbuka, Awamu ya kwanza ya Bonge la mpango mwaka huu tulipata: Mshindi mmoja wa Toyota Fortuner
Watatu wakajinnyakulia TATA Mid- sized Pick-up almarufu kama Kirikuu na wengine 24 walioshinda Lifan 3- wheeler na 120 waliwekewa kiwango cha 100,000 hadi 500,000 kwenye akaunti zao.
Kikubwa zaidi, katika kampeni hii, zaidi ya shilingi Milioni 246 zitatumika kutoa zawadi kwa washindi, huu ukiwa ni mkakati wa Benki hiyo kwa mwaka 2021 ambapo inakusudia kuendelea kuifanya NMB kuwa chaguo namba moja kwa usalama wa fedha za wateja, suluhisho la kifedha na kwa faida.
Wateja wote wa NMB wa sasa na wale watakaofungua akaunti mpya wana nafasi ya kushinda zawadi ya toyo 50 kila moja ikiwa na gharama ya shilingi milioni 4.4.
Lakini pia washindi 120 watajishindia kila mmoja 100,000 jumla ikiwa fedha taslimu shilingi milioni 12, Wateja wanaofungua akaunti za NMB kwa mara ya Kwanza, wakiweka kiasi cha shilingi 100,000, au kuhamisha shilingi 100,000 kutoka kwenye benki zingine na hata mitandao mingine ya simu watajishindia zawadi mbalimbali kutoka NMB kila wiki na kila mwezi.
Kwa wale ambao watafungua akaunti ya NMB au wateja wenye akaunti ya NMB na watakaoweka kiwango cha chini cha shilingi 100,000 kwa muda usiopungua mwezi mmoja, watajiongezea nafasi ya kuingia kwenye droo ya finali itakayochezeshwa mwishoni mwa mwezi Disemba ambapo Toyo 14 zenye thamani ya shilingi Milioni 62 zitatolewa.
Kampeni hii ni ya miezi mitatu inayoanza leo. Katika kipindi hiki cha mavuno kwa wateja wetu, tunatoa fursa pia kwa watanzania wote kufungua akaunti kwetu ili kuingia kwenye orodha ya washindi na pia kupata fursa ya kutunza akiba kwa njia salama zaidi na NMB.
NMB inasema Huu ndiyo Bonge La Mpango awamu ya pili kwa Mwaka huu.