Home Mchanganyiko RC TABORA AAGIZA MA-DC KUHAKIKI MIUNDOMBINU YA SHULE ZOTE

RC TABORA AAGIZA MA-DC KUHAKIKI MIUNDOMBINU YA SHULE ZOTE

0

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani akifungua semina jana mjini Nzega iliyohusu mradi wa kuboresha elimu ndani na nje ya mfumo rasmi wa shule ujulikanao kama Kijana jitambue unaotekezwa kwenye Halmashauri za Wilaya Nane za Mikoa ya Tabora na Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akitoa salamu za Mkoa wake wakati wa kufungua jana semina kuhusu mradi wa kuboresha elimu ndani na nje ya mfumo rasmi wa shule ujulikanao kama Kijana jitambue unaotekezwa kwenye Halmashauri za Wilaya Nane za Mikoa ya Tabora na Shinyanga.

Baadhi ya washiriki wa semina kuhuusu mradi wa kuboresha elimu ndani na nje ya mfumo rasmi wa shule ujulikanao kama Kijana jitambue unaotekezwa kwenye Halmashauri za Wilaya Nane za Mikoa ya Tabora na Shinyanga wakiwa katika semina ya siku moja jana mjini Nzega.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani(mwenye kipaza sauti)  akitoa elimu kuhusu umuhimu wa chanjo ya kujikinga na UVIKO 19 jana kwa Wafanyabiashara katika Mnada wa Ushirika wa Mjini Nzega jana.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani (mwenye kitambaa kichwani) akiangalia Kondoo baada ya kumaliza somo la elimu kuhusu umuhimu wa chanjo ya kujikinga na UVIKO 19 jana kwa Wafanyabiashara katika Mnada wa Ushirika wa Mjini Nzega jana.

Baadhi ya Ng’ombe walioko katika mnada wa Ushirika Mjini Nzega jana.

……………………………………………………………

NA TIGANYA VINCENT

RS TABORA

MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amewagiza Viongozi wa Wilaya zote kupita katika vijiji vyote kwa ajili ya kuhakiki miundombinu ya shule zote ili kuhakikisha hakuna mapungufu ambayo yanaweza kuathiri utoaji elimu bora kwa wanafunzi.

Alisema hatua hiyo itasaidia kubaini mapungufu mapema na kuchukua hatua ya kuondoa dorsari kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi kujifunzi na walimu kufundishia.

Balozi Dkt. Batilda alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua mradi wa kuboresha elimu ndani na nje ya mfumo rasmi wa shule ujulikanao kama Kijana jitambue unaotekezwa kwenye Halmashauri za Wilaya Nane za Mikoa ya Tabora na Shinyanga.

“Tusisubiri vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ituonyeshe mapungufu na ndio tukimbizane kuyatafutia ufumbuzi…ni jukumu la kila Mkuu wa Wilaya , Mkurugenzi na Watendaji wengine kujua matatizo mapema yanayokwamisha utoaji wa huduma kwa jamii …tutaanza kushikana mashari na magauni mambo yakitokea tena kama yalitokea Igunga na Sikonge ya kuonyesha Mwalimu kuishi katika nyuma isiyofaa na watoto kusomea katika Kibanda kilichojengwa katika eneo hatarishi”alionya.

Aliagiza kila Halmashauri lazima iwe na Benki ya Tofali na Madwati ili kuepuka wanafunzi kusomea nje, wengine kukaa chini na walimu kuishi katika nyumba za tembe na wengine mbali na shule wanazofundishia.

Balozi Dkt. Batilda alisema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Haasan imetoa fedha nyingi kwa Mkoa wa Tabora kwa ajili ya Sekta ya elimu  kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu na uboreshaji wa sekta ya elimu.

Alisema kupitia tozo imetoa kiasi cha milioni 462.5 , kupitia mradi wa lipa kwa Matokeo (EP4R) awamu ya nane imetoa bilioni 4.1, na awamu ya tisa imetoa bilioni 3.4 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya madarasa.

Balozi Dkt. Batilda alisema Serikali pia imetoa milioni 801,9 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule za Msingi na Sekondari.

Alisema nje ya fedha hizo kuna kiasi cha shilingi milioni 756.8 ambazo zimetolewa na Serikali kwa ajili ya elimu bila malipo kwa shule za Msingi na Sekondari.

Balozi Dkt. Batilda alisema kupitia fedha hizo ukichanganya na nguvu za wananchi na fedha za Halmashauri haipaswi wanafunzi wasomee nje na wengine wakae chini.