Meneja Masoko na Uhusiano wa STAMICO Geofrey Meena (kulia) akizungumza mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makiragi (katikati) alipotembelea Banda la STAMICO akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel kwenye Maonesho ya nne ya Sekta ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika kwenye uwanja wa Bombambili Mjini Geita.(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule
Mjiolojia kutoka STAMICO Agrey Gonde (wa pili kushoto) akizungungumza mbele ya Mgeni rasmi kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo ikiwemo utafiti wa Madini.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule akiangalia Mbale ya dhahabu kutoka katika Mgodi wa mfano wa Lwamgasa na kusikiliza maelezo ya namna Mgodi huo unavyofanya Shughuli zake kutoka kwa Mjiolojia wa STAMICO Agrey Gonde (kushoto).
Mkuu wa Mkoa wa Geita akiwa na mgeni wake Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana na Nyang’hwale na viongozi wengine katika picha ya pamoja na watumishi wa STAMICO mara baada ya kumaliza kutembelea Banda la Taasisi hiyo kwenye Maonesho hayo.
Afisa Rasilimali watu wa STAMIGOLD Biharamuro Muhunda Nyakiroto (wa pili kushoto) aakielezea namna Taasisi yao inavyotekeleza Shughuli zake.
…………………………………..
Na: Mwandishi wetu, GEITA.
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limesema kuwa kuwepo kwa kiwanda cha kusafisha dhahabu cha Metals Refinery Limited (MPMR) kilichopo Jijini Mwanza kumeleta faida kubwa katika Taifa ikiwemo kupatikana kwa ajira kwa watanzania
Hayo yamesemwa na Mhandisi Uzalishajishaji wa Kiwanda hicho mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makiragi aliyetembelea Banda la STAMICO akimuwakilisha Mkuu wa Mka wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel kwenye Maonesho ya Sekta ya Madini yanayoendelea katika uwanja wa Bombambili MjiniGeita.
Ameeleza kuwa Kiwanda hicho kilichopo katika Wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza kina uwezo wa kusafisha dhahabu kwa 99.99% na kwamba zaidi ya watu 100 wamepata ajira kwenye kiwanda hicho.
“Uwepo wa Kiwanda hiki kimeleta faida nyingi ikiwemo Ajira, Teknolojia Mpya kimekuwa na Fursa kwa makampuni ya ndani kuweza kutoa huduma za uzabuni Kiwandani haapo, pamoja na Wilaya husika kupata tozo mbalimbali kutoka katika kiwanda hicho” Amesema.
Kwa upande wake Afisa Rasilimali watu wa Kampuni ya uchimbaji wa dhahabu iliyopo Biharamuro (STAMIGOLD Biharamuro) Muhunda Nyakiroto ameelezea shughuli za uchimbaji na usalama ikiwemokutoa elimu ya usalama migodini sambamba na kushiriki katika kutoa huduma mbalimbali za kijamii.
Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule na wageni alioambata nao Meneja Masoko na Uhusiano wa STAMICO Geofrey Meenaamesema kuwa katika maoneshohayo wamejikita katika kutoa elimu kwa wananchi kufahamu shuguli zinazofanywa na Shirika lao pamoja na Bidhaa mbalimbali wanazozalisha ikiwemo Mkaa Badala wa Makaa ya Mawe ambao utatumika kwa matumizi ya Nyumbani.