Home Siasa CCM ,ACT WAZALENDO KUCHUANA UCHAGUZI KATA YA NDEMBEZI SHINYANGA

CCM ,ACT WAZALENDO KUCHUANA UCHAGUZI KATA YA NDEMBEZI SHINYANGA

0

Victa Tobias ccm ameteuliwa

…………………………………………………….

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu za kuwania nafasi ya udiwani katika uchaguzi mdogo kata ya Ndembezi limehitimishwa leo ambapo wagombea wawili kati ya 11 waliochukua fomu wameteuliwa kuviwakirisha vyama vyao kwenye kinyang’anyiro hicho.

Msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Ndembezi Bw.Timothy Andrew amewataja walioteuliwa kuwa ni  Mvano Abdul Idd wa chama cha ACT wazalendo na Victor Tobias Mmanywa  wa chama cha mapinduzi CCM,baada ya kukidhi matakwa ya kikanuni ya tume ya uchaguzi ikiwemo kuchukua na kurudisha fomu kwa wakati uliopangwa
Afisa huyo amevitaja vyama tisa ambavyo wagombea wake hawakufanikiwa kurudisha fomu
“Bwana Abdallah Sube wa Chama cha Demokrasia Makini,Rehema Mjengi (ACD), Antony Ndida (SAU), Ramla Shija (NLD), Fatuma Ally (UMD), Emiliana Malema CCK, Ibrahim juma (CHAUMA), Lwitakubi Kabugulu (NRA), Amen Isangi (DP)
Msimamizi huyo wa uchaguzi amesema hatua inayofuata baada ya uteuzi wa majina ya wagombea ni wananchi kuweka pingamizi zoezi ambalo litahitimishwa kesho saa kumi ili kuruhusu hatua nyingine za mchakato wa uchaguzi kuendelea
Aidha Timothy amesema kikao kilichowateua ni kikao cha wasimamizi wa uchaguzi ambapo ametoa wito kwa wananchi kwa yeyote mwenye pingamizi juu ya hao walioteuliwa ofisi ziko wazi ndani ya muda uliopangwa