Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo, Oktoba 5, 2026, amefanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Vietnam, Mhe. Nguyen Hong Dien, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), kando ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

Viongozi hao wamejadili namna ya kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Vietnam na kupanua ushirikiano wa kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili.