*****************************
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul (Mb) Julai 17, 2021 anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye mahafali ya kumi (10) ya Chuo Cha Maendeleo ya Michezo Malya, Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza.
Katika mahafali hayo jumla ya wanachuo 106 wanahitimu ambapo kati ya hao wanachuo 81 ni wanaume na 25 ni wanawake.
Wanachuo hawa wanahitimu kwenye kozi za Stashahada ya Elimu katika Michezo (Ordinary Diploma in Physical Education and Sports) wanachuo 41, Stashahada ya Elimu ya Ufundishaji Michezo (Ordinary Diploma in Sport Coaching Education) wanachuo 23, na Stashahada ya Uongozi na Utawala katika Michezo (Ordinary Diploma in Sports Management and Administration) wanachuo 42.
Asilimia 99 ya wahitimu wa chuo hiki ni walimu kutoka katika halmashauri mbalimbali nchini.
Katika Mwaka wa Fedha 2020/2021 chuo kimetoa mafunzo kwa wadau wapatao 1,445 ambapo kimevuka lengo lake la kutoa mafunzo kwa wastani wa wadau 300 kila mwaka kwenye vituo vyake vya Dar es salaam, Malya na Tunduru.
Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya ni kituo bora cha umahiri wa michezo (center of sports excelency) kinachokuza na kuendeleza vipaji vya michezo nchini, na kujenga weledi wa mafunzo yanayotolewa kwa manufaa ya jamii ya watanzania.