Home Biashara KAMPUNI YA HAMIDU CITY PARK YAINGIA MAKUBALIANBO NA KAMPUNI YA BIMA FIRST...

KAMPUNI YA HAMIDU CITY PARK YAINGIA MAKUBALIANBO NA KAMPUNI YA BIMA FIRST ASSURANCE

0

Mkurugenzi wa Kampuni ya Bima First Assurance Bw.Rogation Selengia akizungumza katika hafla ya kutia saini ya makubalino nyumba zote zinazojengwa na Hamidu City Park kukatiwa bima ya makazi. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Hamidu City Park Bw.Hamidu Mvungi akizungumza katika hafla ya kutia saini ya makubalino nyumba zote zinazojengwa na Hamidu City Park kukatiwa bima ya makazi. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Hamidu City Park Bw.Hamidu Mvungi (kulia) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bima First Assurance Bw.Rogation Selengia wakisaini mkataba wa makubalino nyumba zote zinazojengwa na Hamidu City Park kukatiwa bima ya makazi. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Hamidu City Park Bw.Hamidu Mvungi (kulia) akibadilishana mikataba na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bima First Assurance Bw.Rogation Selengia katika hafla ya kutia saini ya makubalino nyumba zote zinazojengwa na Hamidu City Park kukatiwa bima ya makazi. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Hamidu City Park Bw.Hamidu Mvungi (kulia) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bima First Assurance Bw.Rogation Selengia wakionesha mikataba hafla ya kutia saini ya makubalino nyumba zote zinazojengwa na Hamidu City Park kukatiwa bima ya makazi.

************************

NA EMMANUELMBATILO,DAR ES SALAAM

Kampuni ya Hamidu City Park inayojihusisha na Ujenzi pamoja na uuzaji wa Nyumba iliyopo Wilayani Kigamboni Jijini Dar es Salaam imeingia makubaliano na Kampuni ya Bima ya First Assurance kwaajili ya kuhakikisha nyumba zote zinazojengwa na kampuni hiyo zinakatiwa bima.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni  ya Hamidu City Park Bw.Hamidu Mvungi amesema kuwa watakaonunua nyumba katika eneo hilo watapata fursa ya kupata bima ya makazi.

“Tumeamua kuingia makubaliano na kampuni  ya bima kwa njia nzuri tu kwa maana kumfanya mwananchi ambaye atanunua nyumba kwetu awe nae ana bima ya makazi ambayo itamsaidia pindi nyumba yake ityakapopata majanga”. Amesema Bw.Mvungi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Bima First Assurance Bw.Rogation Selengia amesema kuwa katika kuingia makubaliano hayo ni kuonesha ni jinsi gani ambavyo wanaweza kuwahudumia wananchi katika huduma za bima.

“Tumeona tuwafikie wananchi ambao wapo kwenye nyumba za kampuni ya Hamidu City Park ili tuweze  kuwalinda na majanga yatakayotokea katika nyumba hizo”. Amesema Bw.Selengia.

Aidha Bw.Selengia amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuelewa umuhimu wa bima ili waweze kujiepusha na majanga huku akisema wengi wao hawana elimu ya bima na ndo maana si rahisi  wao kushawishika kuingia  katika huduma za bima.