Home Mchanganyiko KUMBILAMOTO AZINDUA TAASISI YA MTANDAO WA WANAWAKE KWENYE SEKTA YA NISHATI (TAWOE)

KUMBILAMOTO AZINDUA TAASISI YA MTANDAO WA WANAWAKE KWENYE SEKTA YA NISHATI (TAWOE)

0

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe.Omari Kumbilamoto  akitazama baadh i ya teknolojia zinazofanywa kupitia nishati katika hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Mtandao wa Wanawake kwenye Sekta ya Nishati (TAWOE) na programu mpya zilizopo katika Taasisi hiyo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe.Omari Kumbilamoto akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Mtandao wa Wanawake kwenye Sekta ya Nishati (TAWOE) na programu mpya zilizopo katika Taasisi hiyo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Taasisi ya TAWOE Mhandisi Gwaliwa Mashaka akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Mtandao wa Wanawake kwenye Sekta ya Nishati (TAWOE) na programu mpya zilizopo katika Taasisi hiyo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Mshairi Bi.Kanozo Shirima akitoa shairi lake katika hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Mtandao wa Wanawake kwenye Sekta ya Nishati (TAWOE) na programu mpya zilizopo katika Taasisi hiyo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe.Omari Kumbilamoto akizindua Taasisi ya Mtandao wa Wanawake kwenye Sekta ya Nishati (TAWOE) na programu mpya zilizopo katika taasisi hiyo leo Jijini Dar es salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya TAWOE Mhandisi Gwaliwa Mashaka

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe.Omari Kumbilamoto akipata picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa nishati katika hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Mtandao wa Wanawake kwenye Sekta ya Nishati (TAWOE) na programu mpya zilizopo katika Taasisi hiyo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam  

Wadau mbalimbali wakifuatilia hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Mtandao wa Wanawake kwenye Sekta ya Nishati (TAWOE) na programu mpya zilizopo katika Taasisi hiyo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

****************************

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe.Omari Kumbilamoto amezindua Taasisi ya Mtandao wa Wanawake kwenye Sekta ya Nishati (TAWOE) na programu mpya zilizopo katika taasisi hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo Mhe.Kumbilamoto  amewataka wanawake waliopo katika sekta za nishati kujiamini na kufanya kazi kwa weledi huku wakitakiwa kutokukata tamaa ili kuweza kukuza sekta ya nishati hapa nchini.

Amesema atahakikisha anakuwa mstari wa mbele kuisaidia taasisi hiyo ambayo  imeonesha nia ya dhati kuinua wanawake katika sekta ya nishati na kuweza kutatua changamoto mbalimbali.

“Katika kuunga mkono TAWOE ameahidi kuisaidia taasisi hiyo katika kutatua changamoto zinazoikabili huku akiweka wazi kuwa tayari jiji limekwisha tenga asilimia Nne ya mapato yake kwenda kwa kina mama”. Amesema Mhe.Kumbilamoto.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya TAWOE Mhandisi Gwaliwa Mashaka  amesema kupitia uzinduzi huo utasaidia kuwawezesha wanafunzi hasa wakike katika  kuonyesha kile wanachokifanya.

Nae mmoja wa washiriki ambaye ni mshauri muelekezaji masuala ya umeme  kutoka katika kampuni  ya Gein Energy  Product  Farm Dkt.Juliana Palangyo amesema wanawake wengi wapo katika sekta za nishati na wanajitahidi kwa weledi mkubwa huku changamoto kubwa ikionekana ni kutokukubalika.