MWENYEKITI wa Kamati ya uchaguzi wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NaCoNGO ) Wakili Fraviana Charles (kulia) akiwa na katibu Mtendaji wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga (kushoto) wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari kuelekea Uchaguzi Mkuu huo uliofanyika leo Julai 6,2021 Jijini Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Kamati ya uchaguzi wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NaCoNGO ) Wakili Fraviana Charles Akizungumzia mchakato mzima wa uchaguzi
Katibu Mtendaji wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) juu ya mchakato mzima wa kuwapata viongozi wa Wilaya na Mikoa wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NaCONGO ) na kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 8, Julai, 2021.
MWENYEKITI wa Kamati ya uchaguzi wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NaCoNGO ) Wakili Fraviana Charles (kulia) akiwa na katibu Mtendaji wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga (kushoto) wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari kuelekea Uchaguzi Mkuu huo uliofanyika leo Julai 6,2021 Jijini Dar es Salaam.
Na: Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM.
MWENYEKITI wa Kamati ya uchaguzi wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NaCONGO ) Fraviana Charles ametangaza kuwa julai 8 utafanyika uchaguzi ngazi ya Taifa wa baraza hilo.hatua hiyo imekuja baada ya kukamilika kwa chaguzi ngazi ya Wilaya ,mikoa na mashirika.
Amesema kuwa Katika chaguzi za ngazi za Wilaya ,mikoa chaguzi zimefanyika kwa mafanikio makubwa na kazi kubwa iliyobaki ni kuchagua viongozi ngazi ya Taifa nakwamba mkutano huo utafanyika Katika ukumbi wa Royal Village Jijini Dodoma.
Fraviana ameyasema hayo leo mbele ya waandishi wa habari ambapo amesema kuwa yeye Kama mwenyekiti Jukumu lake kubwa ni kuratibu na kusimamia uchaguzi wa Baraza la Taifa Mashirika yasiyokuwa yaserikali .
Amesema Baraza litakalo undwa litakuwa wawakilishi au wajumbe 30 kati ya hao wajumbe 26 kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na mjumbe mmoja kutoka kila mkoa na wajumbe wanne watachaguliwa kutoka Katika Makundi maalum.
Amefafanua kuwa Makundi hayo ni pamoja na mashirika ya kimataifa ,watu wenye ulemavu na watoto pamoja na Vijana .ambapo pia ametumia mkutano huo na waandishi wa habari kutoa taarifa ya matokeo ya uchaguzi wa baraza la Taifa la mashirika yasiyokuwa ya serikali Katika ngazi ya Wilaya uliofanyika Juni 26 2021.
Fraviana amesema kwa ujumla mchakato wa uchaguzi wa wajumbe wa NaCONGO Katika ngazi ya Wilaya ,Mikoa na wa Makundi maalumu ulifanyika kwa mafanikio makubwa mpaka kufikia hatua ya kupata rasmi wajumbe wote wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali( NaCONGO )
“Tunatarajia uchaguzi Katika ngazi ya Taifa utafanyika pia kwa weledi na mafanikio makubwa ili tuweze kupata viongozi wa baraza jipya yaani Mwenyekiti ,Katibu mkuu pamoja na mweka hazina wa Baraza.”amesema Fraviana.
Amefafanua kuwa baada ya uchaguzi Julai 8 siku inayofuata Julai 9 wataapishwa viongozi wapya wa kitaifa na Julai 10 viongozi wapya watakabidhiwa nyaraka na ofisi kutoka kwa uongozi waliomaliza muda wake .
Akizungumzia uchaguzi wa ngazi za Wilaya ,Mikoa na mashirika katibu Mtendaji wa kamati ya uchaguzi ambaye pia ni mkurugenzi Mtendaji wa FCs amesema Katika mchakato wa uchaguzi huo uliopita changamoto zilikuwepo lakini wanashukuru wamemaliza salama na Sasa wanakwenda kumaliza kazi Katika ngazi hiyo ya Taifa.