Leo Julai 3, 2021 Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Dkt.Mussa Budeba , ameipongeza Wizara ya Madini, Taasisi zake pamoja na wadau wengine walio katika Banda la Wizara hiyo kwa namna wanavyoendelea kuwahudumia wananchi na wadau wengine katika Maonesho ya 45 ya Biashara maarufu Kwa jina la Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam.
Dkt.Budeba aliweza kutembelea mabanda mbalimbali ndani ya Banda la Wizara ya Madini.
Akiwa katika Banda la GST Dkt.Budeba alipata fursa ya kuona namna wataalam wa GST wanavyoendelea kuwahudumia wadau mbalimbali waliotembelea banda hilo.
Akizungumza na wadau waliofika katika Banda la GST Dkt.Budeba aliwapongeza kwa kutembelea banda la GST ili kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu utafutaji wa madini na huduma zitolewazo na GST kwa ujumla. Vilevile, aliwaalika wadau mbalimbali kutembelea banda la GST ili kufahamishwa madini yanayopatikana nchini Tanzania. Aidha, aliwaalika wadau mbalimbali kuitumia GST ili kuongeza tija na uzalishaji katika shughuli zao za utafutaji, uchimbaji na uchenjuaji madini.
Maonesho haya yanatarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 5/7/2021.
Zifuatazo ni picha mbalimbali zinazomuonesha alipotembelea katika mabanda hayo leo.