Home Biashara WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA BOT SABASABA

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA BOT SABASABA

0

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo akitia saini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Umma, Bi. Beatrice Ollotu. 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo, akipewa maelezo na Afisa Uhusiano wa Umma, Bi. Beatrice Ollotu, kuhusu elimu na huduma zinatolewa katika banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo, akizungumza na Mchambuzi wa Masuala ya Fedha Mwandamizi, Bw. Ephraim Madembwe kuhusu Dhamana za Serikali alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo, akipewa maelezo kuhusu Dawati la Utatuzi  wa Malalamiko ya Wateja wa Huduma za Kibenki alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo, akipewa maelezo na Afisa Uhusiano wa Umma, Bi. Beatrice Ollotu, kuhusu Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania Mwanza.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo, akipewa maelezo na Afisa Benki Mkuu Mwandamizi, Bi. Restituta Minja,  kuhusu uchakataji wa noti alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.