Mwanji Mbaka Mhandisi Mjenzi Mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea katika banda la Shirika la Umeme Tanzania TANESCO katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mwanji Mbaka Mhandisi Mjenzi Mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) amekuwa akitoa maelezo mbalimbali kwa wananchi wanaotembelea kwenye banda la TANESCO jinsi mradi wa Julius Nyerere Hydro Power Project unavyotekelezwa kwa ustadi mkubwa na kasi.
Hii inawasaidia wananchi ili kupata uelewa na kujua jinsi serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mh. Samia Suluhu Hassan inavyotekeleza miradi ya maendeleo ambayo hapo baadaye italeta tija kubwa katika uchumi wa Tanzania.
Bwawa la Umeme la JNHPP linatarajiwa kuzalisha Megawati 20115 wakati litakapokamilika na kuongeza kasi ya maendeleo ya viwanda, Teknolojia na kilimo kote nchini na kuufanya uchumi wa Tanzania kuimarika zaidi katika miaka ijayo. Picha mbalimbali chini zikionesha baadhi ya wananchi mbalimbali waliotembelea kwenye banda la Shirika la Umeme Tanzania TANESCO katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.