Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo katika nyakati tofauti leo amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama Tawala Cha Burundi cha CNDD-FDD Ndg. Reverien Ndikuriyo na Balozi wa Namibia nchini Tanzania Ndg. Lebius Tangeni Tobius.
Mazungumzo hayo yemefanyika leo tarehe 10 Juni, 2021 katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM Dodoma.
katika mazungumzo ya awali, Katibu Mkuu wa Chama tawala Cha Burundi CNDD-FDD amesifu uhusiano mzuri uliopo na Chama Cha Mapinduzi na amesisitiza kuuendeleza na kuendelea kujifunza zaidi kupitia uzoefu mzuri wa uongozi uliopo ndani ya CCM.
Aidha, Katibu Mkuu wa CCM katika mazungumzo hayo, amemuhakikishia Katibu Mkuu wa CNDD-FDD kuwa, CCM itaendelea kuimarisha uhusiano mzuri uliopo na kuendeleza mshikamano, urafiki na undugu wa kihistoria.
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa CCM akizungumza na Balozi wa Namibia nchini, wote kwa pamoja wameendelea kuweka mkazo uhusiano mzuri uliopo kati ya Nchi ya Tanzania na Namibia na Chama Tawala cha Namibia SWAPO na Chama Cha Mapinduzi.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na baadhi ya viongozi Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa (NEC) akiwemo Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Ngemela Lubinga, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Mwl. Raymond Mwangala.
Huu ni muendelezo wa Katibu Mkuu kukutana na kuzungumza na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuendelea kuimarisha uhusiano mzuri uliopo na kujifunza zaidi.
Imetolewa na;
Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI