Home Mchanganyiko ZIARA YA MBUNGE HOSPITAL YA WILAYA YA CHUNYA.

ZIARA YA MBUNGE HOSPITAL YA WILAYA YA CHUNYA.

0

Mbunge wa Jimbo la Lupa-Chunya mhe Masache Kasaka, leo tarehe 10 June 2021 amefanya ziara ya kutembelea hospital ya Wilaya.

Katika ziara hiyo mhe Mbunge alikagua miundombinu ya hospital na pia alizungumza na watumishi wa afya ili kufahamu changamoto zinazowakabili na kuangalia namna nzuri ya kuzitatua.

Pia mh Mbunge alipata wasaa wa kujionea jinsi wahudumu wa afya wanavyojitahidi kuwahudumia wananchi.

Katika kikao na watumishi, mhe Mbunge amewahimiza kushirikiana ili kuongeza ufanisi….

Pia kwenye udhaifu ameyachukua na akifika bungeni atayawasilisha sehemu husika ili kuchukuliwa hatua za ufumbuzi.

Mhe Mbunge amewapongeza sana watumishi wa idara zote kwa jinsi wanavyoshirikiana vyema na serikali katika kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi ambayo yeye ni mmoja wa wale walioahidi kuitekeleza na kuwaletea maendeleo wananchi.

Kwenye ziara hiyo Mbunge aliongozana na katibu wa Mbunge na watendaji na wakuu wa idara toka halmashauri ya Wilaya.

“Chunya yetu itajengwa na Mimi na wewe,” amesema Mh. Masache Kasaka

Imetolewa na ofisi ya Mbunge Jimbo la Lupa-Chunya..
10-06-2021..