KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ambaye pia ndiyo mlipaji mkuu wa serikali Bw. Emmanuel Tutuba, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wahariri kuhusu ubia wa sekta ya Umma na Binafsi katika utekelezaji wa miradi kwenye ukumbi wa Hazina ndogo wa Wizara ya Fedha jijini Arusha Juni 3, 2020
KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ambaye pia ndiyo mlipaji mkuu wa serikali Bw. Emmanuel Tutuba, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wahariri kuhusu ubia wa sekta ya Umma na Binafsi katika utekelezaji wa miradi kwenye ukumbi wa Hazina ndogo wa Wizara ya Fedha jijini Arusha Juni 3, 2020. Katikati ni Kamishna wa PPP, Dkt.John R. Mboya na Kamishna Msaidizi wa PPP, Bw. Bashiru H. Taratibu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya FEdha na Mipango Bw. Emmanuel Tutuba akimsikiliza Benny Mwang’onda Mwenyekiti wa wahariri katika semina hiyo wakati alipokuwa akitoa shukurani kwa Katibu Mkuu huyo kufungua semina hiyo.
Kamishna wa PPP Wizara ya Fedha na Mipango Dk. John Mboya akitoa mada kuhusu PPP katika semina hiyo ya wahariri wa vyombo vya habari inayofanyika kwenye ukumbi wa Hazina Ndogo jijini Arusha.
Kamishna wa PPP Wizara ya Fedha na Mipango Dk. John Mboya akielezea namna mfumo huo wa PPP unavyofanya kazi wakati wa semina hiyo ya wahariri wa vyombo vya habari inayofanyika kwenye ukumbi wa Hazina Ndogo jijini Arusha.
Picha mbalimbali zikionesha wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali nchini wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa kwenye semina hiyo.
Mablogger Ahmed Michuzi na Khalfan Said wakitekeleza majukumbu yao katika semina hiyo.
Mgeni Rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel Tutuba akiwa katika picha mbalimbaliza pamoja na washiriki wa semina hiyo pamoja na maofisa wa Wizara hiyo.
Katibu mkuu wizara ya fedha na Mipango Bw.Emmanuel Tutuba leo June 03 amefungua Mafunzo ya siku mbili kwa wahariri 38 kutoka vyombo mbalimbali nchini juu ya Utekelezaji wa Miradi kwa Utaratibu wa Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi (PPP).
Akizugumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo hayo yalioanza jijini Arusha ndg.Tutuba amesema kuwa serikali imeandaa Programu ya PPP nchini ili kuwezesha sekta binafsi kushirikiana na Serikali kwa utaratibu wa Ubia kati ya Umma na sekta Binafsi kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta mbali mbali.
Katibu Mkuu Ndg.Tutuba alisema kuwa ili kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa program hii serikali iliweka mipango ya kutekeleza amza hiyo iliyokuwa kuandaa sera ya PPP mwaka 2009,Sheria ya PPP Sura 103,na kanuni za kutekeleza Sheria hiyo ambayo mwelekeo huo unashabiana na mipango iliyowekwa na nchi nyingi za Afrika kutumia sekta binafsi kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleokwa kutumia PPP.
“Ndugu zangu Wahariri dhana hii sio ngeni kwa Tanzania kabla ya kutungwa kwa Sera ya PPP mwaa 2009,serikali ilihusisha Sekta Binafsi kutekeleza baadhi ya miradi nikitaja mifano ya miradi ya IPTL,City Water na RITES – India ambapo miradi hiyo haikufanikiwa kutokana na changamoto ya kukosekana kwa mazingira wezeshi yenye kuelekeza taratibu kabla ya kuingia mikatabaya PPP.”Alisema Ndg.Tutuba
Aidha alisema kuwa Programu ya PPP nchini ina umuhimu mkubwa katika utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Hata hivyo amezitaka mamlaka za Serikali zilizopewa Jukum la kuibua na kutekeleza Miradi ya maendeleo katika sekta inazosimamia zinapaswa kutumia ipasavyo utaratibu wa PPP,kwa mradi yenye sifa za kuihuisha sekta ya binafsi katika kutekeleza baadhi ya miradi ya maendeleo yenye uwezekano wa kuishirikisha sekta binafsi,badala ya kutegemea bajeti za Serikali.
Kwa upande wake Kamishna wa Ubia kati ya sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) Dkt.John Mboya alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kujenga uelewa wa kufahamu utaratibu huo,na kushirikisha sekta binafsi katika kutekeleza miradi ya maendeleo ili kuongeza kasi ya maendeleo nchini.
Dkt.Mboya alisema kuwa utaratibu wa Ubia wa PPP ni njia muhimu sana kwa vyanzo mbadala vya kugharamia miradi ya maendeleo kwa kuwa mapato ya kodi pekee hayatoshelezi kugharamia miradi ya maendeleo.
Hata hivyo alisema kuwa hadi mwezi mei,2021 jumla ya miradi 41 ipo katika hatua mbali mbali za maandalizi ambapo thamani ya miradi katika hatua zote ni inakadiriwa kugharimu shilingi trilioni 3.402 ambapo inaandaliwa katika sekta ya mawasiliano,ujenzi,afya,elimu,biashara na maji.
“Mheshimiwa Katibu Mkuu na Wahariri kabla ya mwaka huu wa fedha jumla wadau 829 walipatiwa elimu hii,na walihusika ni pamoja na watumishi wa Wizara,Idara zinazojitegemea,Taasisi za Umma, Halmashauri, Wabunge, Makatibu Wakuu na Wakurugenzi wa Halmashauri.”Alisema dkt.Mboya.