Home Mchanganyiko WAZIRI WA AFYA DKT.GWAJIMA AFANYA MAZUNGUMZO NA DC. SENDIGA

WAZIRI WA AFYA DKT.GWAJIMA AFANYA MAZUNGUMZO NA DC. SENDIGA

0

*******************************

Dodoma

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga Kwenye ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Viongozi hao wamejadili mwenendo wa utoaji huduma za afya, hali ya watumishi na dawa pamoja na maboresho ya miundombinu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya Katika mkoa wa Iringa.

Katika kikao hicho Mkuu wa aliambatana na Katibu Tawala wa mkoa Bi. Happynes Seneda.