Picha mbalimbali zikionesha mbunge wa Jimbo la Nachingwea Mkoani Lindi Amandus Chinguile akikabidhi msaada wa Saruji kwa jimbo hilo, Zoezi hilo limefanyika katika Viwanja vya Nachingwea Square
huku Viongozi mbalimbali wakihudhuria.
Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Mkoani Lindi Amandus Chinguile akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada wa mifuko ya Saruji kwa jimbo la Nachingwea mkoani Lindi.
……………………………………….
Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Mkoani Lindi Amandus Chinguile ameendelea kutekeleza ahadi zake alizoahidi kwa wananchi wakati akiomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo hilo katika Kampeni ya uchaguzi mkuu 2020.
Mei 22 /2021 Mbunge huyo ametimiza ahadi yake katika sekta ya ELIMU katika kata 16 kwa kugawa mifuko ya saruji 1,800 yenye thamani ya zaidi ya Million 22.
Zoezi hilo limefanyika katika Viwanja vya Nachingwea Square
huku Viongozi mbalimbali wakihudhuria.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo,Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Amandus Chinguile alisema ‘yeye kama Mbunge anao wajibu wa kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira rafiki kwa kuwaboreshea miundombinu.
Alisema kuwa ataendelea kuziangazia shule zenye changamoto na kuziwekea mazingira rafiki ya kujifunzia.
Vifaa hivyo vinatarajia kutumika kakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 22 katika Shule za Sekondari zilizopo Jimboni humo.
“Ni wajibu wetu sisi kama viongozi na wadau mbalimbali kuhakikisha tunashirikiana kwa pamoja kuinua Elimu katika wilaya yetu kwa kuhakikisha tunaiboresha Miundombinu ya shule”Alisema Chinguile.
Aliongeza kuwa,katika hii awamu ya kwanza ni nimeziangazia kata 16 katika sekta ya Elimu,nitaendelea kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika kata zingine ili Jimbo letu liweze kupiga hatua katika Maendeleo kwa kuimarisha miradi ya Maendeleo.
Bado hitaji ni kubwa katika sekta ya Elimu pamoja na sekta nyingine,hivyo ni jukumu la kila mdau kuendelea kuchangia ninawaomba wadau mbalimbali waendelee kujitokeza kuchangia.