***********************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Yanga imeendelea kusumbuliwa na matokeo mabaya katika ligi kuu Tanzania bara baada ya kuambulia pointi moja kwa kutoka sare na Namungo Fc 0-0.
Katika mchezo huo Yanga ilichezea nafasi nyingi za wazi ambazo zingewasaidia kupata ushindi katika mchezo huo japo Namungo nao walionesha nia ya uahindi katika mchezo huo.
Kwa matokeo hayo inaipa nafasi nzuri klabu ya Simba ambayo ipo kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika kwenye hatua ya robo fainali ambapo anacheza na klabu ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini.