Home Michezo SIMBA SC YAAMBULIA KIPIGO CHA 4G AFRIKA KUSINI

SIMBA SC YAAMBULIA KIPIGO CHA 4G AFRIKA KUSINI

0

******************

NA EMMANUEL MBATILO

Klabu ya Simba imepokea kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini katika hatua ya kwanza ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba itatakiwa kushinda idadi ya tofauti ya mabao matano katika raundi ya pili ya robo fainali ambayo itachezwa katika uwanja wa Benjamini Mkapa ambapo Simba itakuwa mwenyeji.

Mabao ya Kaizer Chiefs yaliwekwa kimyani na Erick Mathoho dakika ya 6, Samir Nurkovic dakika 34 na dakika 57 wakati bao la mwisho likifungwa na Leonardo Castro dakika 63.