Mkurugenzi wa makampuni ya Otama yanayojishughulisha na ukusanyaji wa taka katika kata ya Moivo Emmanuel Kweka Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasaidia walemavu hao.
Baadhi ya walemavu hao kulia akiwa ni Husna Rmadhani na kushotp akiwa ni temba wakiwaeleza waandishi wa habari sababu za kushindwa kurejesha mkopo waliopewa na halmashauri.
………………………………………………………………..
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Kikundi cha watu wenye ulemavu kata ya Moivo halmashauri ya Arusha DC yenye jumla ya wanachama watano kimesaidiwa kurejesha mkopo waliouchukua wa asilimia 2 za walemavu unaotolewa na halmashauri kutokana na kushindwa kurejesha mkopo huo kwasababu ya changamoto walizokumbana nazo na kuanzishiwa mradi wa kuku 600 huku jamii ikiombwa kuwasaidia.
Msaada huo wa shilingi million moja walioupata kutoka kwa mkurugenzi wa makampuni ya Otama yanayojishughulisha na ukusanyaji wa taka katika kata hiyo Emmanuel Kweka kwa kushirikiana na marafiki zake ambapo alisema kuwa waliona wawasaidi baada ya kusikia wameshindwa kurejesha mkopo wa halmashauri kwa muda mrefu na kwasababu hiyo wanatakiwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Kweka alisema kuwa pamoja na wao kuwasaidia kulipa hicho kidogo pamoja na kuwapa vifaranga vya kuku chotara pia wanaiomba jamii kuwasaidia watu hao ili kuweza kutatua changamoto za kimaishazinazowakabili na kujikwamua kiuchumi.
Pia aliiomba serikali kuwapa watu hao mkopo utakaweza kuwasaidia hata kama wakiyumba kibiashara na kimaisha kwani wanavyowapa mkopo mdogo wanapopita katika changamoto kidogo mkopo huo ambao ni mtaji kwao unateketea wote.
Kwa upende wa baadhui ya walemavu hau Husna Ramdhani na Gimson Ndossi na mmoja aliyetambulisha kwa jina moja la Temba walisema kuwa walichukua mkopo wa shilingi milioni tatu na kila mmoja kupeleka mgao wake katika biashara lakini kutokana na changamoto tofauti tofauti walizopitia mtajio wao ulisha na wakashindwa kurejesha fedha hizo kwa muda uliotakiwa.
Walieleza kuwa changamoto hizo nin pamoja na baadhi yao kuibiwa na wengine kuugua muda mrefu jambo lililopelekea baadhi kukosa mtaji wa kuendeleza biashara zao pamoja na wengine kushindwa kufanyakazi kwasdabubu zaq kiafya.
Aidha waliomba jamii kuendelea kuwaunga mkono ili weweze kumaliza kulipa deni hilo ambalo hadi hivi sasa bado wanadaiwa shilingi milioni moja na nusu huku wakimshukuru mdau huyo ambaye amewasaidia kulipa shilingi milioni moja pamoja na kuwapa mradi mpya wa kuku utakowasaidia kujiingizia kipato.
Sambamba na hayo pia waliiomba serikali kutokata tamaakatika kuwasaidia walemavu kwa wao kuanguka sio mwisho wa maisha ya wengine hivyo iendelee kuwapa walemavu kipaumbele.