Home Mchanganyiko PSSSF SACCOS YATOA MISAADA MBALIMBALI KITUO CHA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM BUIGIRI...

PSSSF SACCOS YATOA MISAADA MBALIMBALI KITUO CHA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM BUIGIRI WILAYANI CHAMWINO

0

Meneja wa PSSSF Saccos,Elizabeth Mushi,akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika  kitu cha Watoto wenye mahitaji maalum ya  Buigiri Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma mara baada ya kutembelea na kutoa misaada mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni mbili.

Baadhi ya wafanyakazi wa  PSSSF Saccos wakishusha mizingo  katika Kituo cha Watoto wenye Mahitaji Maalum kilichopo Buigiri Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma walipotembelea na kutoa misaada ya vitu mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni mbili.

Baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika Kituo cha Watoto wenye Mahitaji Maalum kilichopo Buigiri Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wakisubiri kupokea zawadi kutoka PSSSF Saccos ambao walitembelea shule hiyo na kutoa misaada ya vitu mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni mbili.

Meneja wa PSSSF Saccos,Elizabeth Mushi,akizungumza mara baada ya kutoa Misaada ya vitu mbalimbali yenye thamani ya shilingi Milioni mbili katika kitu cha Watoto wenye mahitaji maalum kilichopo Buigiri Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma .

Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo,Godfrey Daudi,akitoa neno la shukrani kwa Meneja wa PSSSF Saccos,Elizabeth Mushi,mara baada ya kupokea  Misaada ya vitu mbalimbali yenye thamani ya shilingi Milioni mbili katika kitu cha Watoto wenye mahitaji maalum kilichopo Buigiri Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma .

Baadhi ya vitu vilivyotolewa.

Wafanyakzi wa PSSSF Saccos wakiwagawia watoto zawadi mara baada ya PSSSF Saccos,Ekutoa Misaada ya vitu mbalimbali yenye thamani ya shilingi Milioni mbili katika kitu cha Watoto wenye mahitaji maalum kilichopo Buigiri Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma .

Meneja wa PSSSF Saccos,Elizabeth Mushi,akiwa anafurahia na watoto waliopo katika kitu cha Watoto wenye mahitaji maalum ya Buigiri Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma mara baada ya kutembelea na kutoa misaada mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni mbili.

Meneja wa PSSSF Saccos,Elizabeth Mushi,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoa Misaada mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni mbili  katika  kitu cha Watoto wenye mahitaji maalum ya  Buigiri Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma 

………………………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Chamwino

SACCOS ya Mfuko  wa Hifadhi ya Jamii  kwa watumishi wa Umma (PSSSF) imetembelea na kutoa mahitaji mbalimbali ya  chakula,mafuta,sabuni,juice,taulo za kike  na sare za shule  kwa kituo cha Shule ya Watoto wenye mahitaji maalum ya Buigiri Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Akizungumza Mei 12,2021 mara baada ya kutoa mahitaji hayo,katika kijiji cha Buigiri Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma,Meneja wa PSSSF Saccos,Elizabeth Mushi,amesema wamefika katika shule  hiyo  kutokana na wajibu wa Saccos yao kuchangia jamii  na  kusaidia watu wenye mahitaji maalum hivyo wamewapatia vyakula,mafuta, sabuni,juice za watoto,sare za shule taulo za watoto wa kike zenye thamani ya shilingi milioni 2.

Amesema ni mara yao ya kwanza kufanya jambo hilo ambapo amedai kwa sasa utakuwa ni utaratibu wao kila mwaka kusaidia watoto wenye mahitaji maalum katika vituo mbalimbali.

“Hapa ndio tumeanza mara zote hatutaliacha kabisa na sio lazima kiwe kituo hichi tu na  siku nyingine tutaangalia kitu kingine chenye uhitaji.Jambo hili,linatakiwa lifanyike kila mwaka lakini Saccos yetu bado ndogo lakini kwa mwaka huu ndio tumetoa,”amesema.

Amesema jukumu la kutunza watoto wenye mahitaji  ni la kila mmoja hivyo jamii inapaswa kupeleka kidogo kidogo ili kuwapa furaha na kuwafanya wasahau matatizo yao.

“Tunaiambia Serikali jukumu la kutunza watoto kama hawa ni la kila jamii ambayo inauwezo kwa sababu wao wenyewe hawajajitosheleza mahitaji yao lakini kila jamii ikilea kidogo kidogo kwa furaha bila kukumbuka matatizo yao walioyonayo,”amesema.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo,Godfrey Daudi amesema shule hiyo ina wanafunzi 119 ambao ni wasiiona kabisa,wenye uoni hafifu,wenye ulemavu wa ngozi na wa kawaida kwa ajili ya sera ya elimu jumuishi.

Amesema changamoto wanazokabiliwa nazo  ni pamoja na bajeti kutokukidhi kwa sababu matumizi wanayotumia  kwa mwezi ni shilingi  milioni tatu kwa ajili ya bili za umeme,maji,chakula  na matibabu kwa wanafunzi.

Hata hivyo,anasema mahitaji yao  kwa mwezi ni shilingi  milioni 8 hivyo wanamuomba Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan awasaidie ili waweze kuwasaidia wanafunzi waliopo katika shule hiyo.

“Kwa kushirikiana na Serikali yetu inayoongozwa na mama yetu Mama Samia Suluhu Hassan ambaye tunamuombea usiku na mchana kwa manufaa ya Taifa letu sisi bajeti yetu ni shilingi milioni 8 kwa mwezi  na tunamuomba mama yetu aliangalie hili tunajua atafanya,”amesema.

Mwalimu huyo aliishukuru PSSSF Saccos kwa misaada waliyoitoa huku akizitaka Taasisi na Mashirika mengine ya umma kuiga mfano wa mfuko huo.

“Kwanza niwashukuru kwa mamna wanavyotoa sapoti niwaombe waongeze nguvu kwa sababu namna hawa walivyo ni mapenzi ya mungu na hakuna walichomkosea mungu.Natamani sana suala la bajeti na kwa hilo nikuishukuru Serikali kwa sababu inaunga mkono inafanya mambo makubwa sana kwenye hii shule kwa sababu inafanya ujenzi wa bweni lenye thamani ya shilingi milioni 80,”amesema.

Naye, Dada Mkuu wa shule hiyo,Lucy Michael ameiomba jamii izidi kuwatembelea watu wenye ulemavu na wenye  mahitaji maalum huku akidai ndoto yake ni kuwa mtangazaji katika siku za baadae.