Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akifungua mafunzo ya elimu ya matumizi sahihi ya vipimo kwa wazalishaji na wafungashaji wa bidhaa mbalimbali katika Mkoa wa Singida yaliyofanyika katika ukumbi wa Bishop Rwoma Singida mjini, Leo Aprili 28,202.
Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa Wakala wa Vipimo, Bw. Deogratias Maneno akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi zawadi ya mizani iliyotengenezwa hapa nchini na kuhakikiwa na Wakala wa Vipimo mara baada ya kufungua mafunzo ya elimu ya matumizi sahihi ya vipimo kwa wazalishaji na wafungashaji wa bidhaa katika mkoa wa Singida yaliyofanyika katika ukumbi wa Bishop Rwoma Singida mjini, Leo Aprili 28,2021
Ally S. Mwendo aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya akikabidhi cheti kwa mjasiliamali baada ya mafunzo ya elimu ya matumizi sahihi ya vipimo kwa wazalishaji na wafungashaji wa bidhaa katika Mkoa wa Singida yaliyofanyika katika ukumbi wa Bishop Rwoma Singida mjini, Leo Aprili 28,2021 Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa Wakala wa Vipimo, Bw. Deogratias Maneno na wazalishaji na wasindikaji wa bidhaa mbalimbali baada ya ufunguzi wa mafunzo ya elimu ya matumizi sahihi ya vipimo yaliyofanyika katika ukumbi wa Bishop Rwoma Singida mjini, Leo Aprili 28,2021.
Maafisa kutoka Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) wakitoa elimu ya matumizi sahihi ya vipimo kwa wazalishaji na wafungashaji wa Mkoa wa Singida yaliyofanyika katika ukumbi wa Bishop Rwoma Singida mjini, Leo Aprili 28,2021
Picha zote na Eliud Rwechungura
*******************************
Wazalishaji na Wafungashaji wa bidhaa katika Mkoa wa Singida watakiwa kuzingatia elimu ya matumizi sahihi ya vipimo ili waweze kurudisha imani kwa watumiaji wa bidhaa zao na kuimalisha masoko ya ndani na nje ya nchi na hivyo kujenga uchumi wa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla.
Ameyaeleza hayo, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi wakati wa akifungua Mkutano wa utoaji wa elimu ya matumizi sahihi ya vipimo kwa wazalishaji na wafungashaji wa bidhaa ulioandaliwa na Wakala wa Vipimo (WMA) katika ukumbi wa Bishop Rwoma – Singida mjini leo Aprili 28, 2021.
‘‘Elimu ya matumizi ya vipimo sahihi itakayotolewa leo itakuwa msaada mkubwa kwetu sote na Taifa kwa ujumla ukizingatia tunatumia vipimo kufanikisha mambo mbalimbali yanayotuzunguka; iwe kwenye ujenzi, afya, mazingira, usalama na katika maeneo tuliyozoea ya kibiashara na bidhaa za mkoani kwetu zitakuwa na vipimo sahihi vitakavyorudisha imani kwa watumiaji wa ndani na nje na kuimalisha soko la bidhaa zenu’’ ameeleza Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi.
Dkt.Rehema Nchimbi ameipongeza Wakala wa Vipimo kwa kuendelea kutambua wajibu wao wa kuendelea kuwatembelea na kuwafikia wananchi kwa kusogeza elimu na mafunzo ya matumizi sahihi ya vipimo katika Mkoa wa Singida na hivyo, amewataka kuendelea kutoa elimu kwa wazalishaji na wafungashaji kila inapobidi ili kuwaondolea vikwazo kwenye shughuli zao za kila siku katika Mkoa wa Singida ili Mkoa uweze kuwa mfano katika matumizi ya vipimo sahihi.
Aidha, Dkt.Rehema Nchimbi ameziagiza halmashauri na manispaa kutenga jengo ambalo litakuwa ni kituo cha kutoa huduma zote kwa wananchi wote ambao ni wazalishaji na wafungashaji ikiwemo huduma ya vipimo na huduma nyingine zinazowiana ili wananchi wanapokuja waweze kupata huduma zote sehemu moja.
Dkt.Rehema Nchimbi ametoa wito kwa washiriki wa mafunzo hayo kuwa mfano katika kutekeleza masuala yote yanayohusiana na vipimo watakayofundishwa na baada ya mafunzo hayo, bidhaa za Mkoa wa Singida ziwe na vipimo sahihi vitakavyorudisha imani kwa watumiaji wa ndani na nje na kuimalisha soko la bidhaa zenu za Mkoa na nchi kwa ujumla.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa Wakala wa Vipimo Bw. Deogratias Maneno ameeleza kuwa mafunzo hayo ni mwendelezo wa utoaji wa elimu ya vipimo katika Mikoa yote nchini na kwa Mkoa wa Singida yamelenga kutoa elimu ya vipimo kwa wazalishaji, wafungashaji, wauzaji wa mafuta ya alizeti, unga pamoja na wasindikaji wa asali.
Bw. Deogratias Maneno ameeleza kuwa kipimo sahihi ni nyenzo muhimu katika kubadilishana bidhaa na fedha, ili biashara ifanyike kwa haki lazima vipimo sahihi vitumike, mfano mtu anayefungasha bila kufuata matakwa ya Sheria ya Vipimo anaweza kuzidisha au kupunguza ujazo/uzito wa bidhaa. Kuzidisha vipimo kunampa hasara mwenye mali (mtengenezaji) na kumfanya asipige hatua katika biashara yake, wakati kupunguza kunasababisha mnunuzi kupata bidhaa pungufu ya pesa aliyotoa.
Naye, Maliam Mohamed, Mjasiliamali kutoka Ikungi Singida ameshukuru Wakala wa Vipimo kwa elimu waliyoitoa kwao ambayo itakuwa msaada mkubwa katika biashara zao na itawasaidia kufanya biashara kwa uaminifu, uhuru na kujiamini na hiyo itawafanya kusafirisha bidhaa katika Mikoa mingine kwa sababu watakuwa na uhakika wa vipimo sahihi nah ii itawasaidia kuondokana na adhabu ya faini au kifungo kama Sheria ya vipimo inavyosema.