Home Biashara TECNO CAMON KUZALIWA UPYA NA SELFIE YA MP48.

TECNO CAMON KUZALIWA UPYA NA SELFIE YA MP48.

0

Ubora wa MP 48 za selfie Kamera na 4k video resolution Kuja kufunika simu zote ambazo kwa sasa zinasemekana kuwa simu bora katika soko la simu. Tangu kuanza kwa Mwaka huu wa 2021 Kampuni ya simu TECNO imekuwa kimya na sasa mbioni kuuvunja ukimya huo na kitu kipya kabisa kipya kutoka kwenye series pendwa ya TECNO Camon.

Series ya TECNO Camon imekuwa ikiaminika kuwa na simu zenye kamera kali kutoka kwenye kampuni hiyo, japo simu hiyo haijatambulishwa rasmi lakini tayari kuna tetesi huenda simu hiyo ni TECNO Camon 17 pro. TECNO Camon 17 pro inasemekana kuja kuwa suluhisho kwa wenye uhitaji mkubwa wa kamera katika kazi za kila siku.

Simu hii inayosemekana kuwa camon 17pro ina 4K video resolution hii ni
teknolojia ya hali ya juu sana katika mfumo mzima wa uchukuaji video kuwahi kutokea TECNO.

Camon mpya inasemekana kuja kutunufaisha wapenzi wa games na wafanyakazi wa maofisini hasa wale wenye kuhitaji nguvu ya processor wakati wa utendaji wa kazi.

Ufanisi wa processor ya Helio G85 huyatenda yote hayo pasipo hitilafu ya simu kupata joto.

Camon 17pro huenda uwezo wa kuhifadhia kumbukumbu ukawa ni mkubwa zaidi kama si 256ROM kwa 8RAM basi ni 128ROM kwa 8RAM na si vyenginevyo.

Lisemwalo lipo kama halipo linakuja wapenzi wa simu za TECNO tuanze kujichanga vile vile Kwa mengi zaidi na yenye uhakika kuhusu ujio wa TECNO Camon tusikae mbali na @tecnomobiletanzania. www.tecno-mobile.com