Home Mchanganyiko MCHUNGAJI WA KANISA LA BAPTIST NYANHENDE AMWAGA MSAADA KWA WATOTO WENYE UALBINO...

MCHUNGAJI WA KANISA LA BAPTIST NYANHENDE AMWAGA MSAADA KWA WATOTO WENYE UALBINO BUHANGIJA

0

 


 

Mchungaji wa Kanisa la Baptist Nyanhende Manispaa ya Shinyanga Renatus Kanunu, akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto wenye mahitaji maalumu wanaolelewa kituo cha Buhangija , kikiwemo chakula.

 

Na Marco Maduhu, Shinyanga.
Mchungaji wa Kanisa la Baptist lililopo Nyanhende Manispaa ya Shinyanga Renatus Kanunu, ametoa msaada wa vitu mbalimbali kikiwamo chakula na vifaa vya michezo kwa watoto wenye mahitaji maalumu, ambao wanalelewa katika kituo cha Buhangija jumuishi.
 
Akizungumza  leo Aprili 28,2021 wakati akikabidhi msaada huo, amesema jamii inapaswa kuguswa kusaidia watoto hao, ili kuwaondolea changamoto ambazo zinawakabili.
 
Amesema yeye kama mchungaji ameguswa na watoto hao wenye mahitaji maalumu, na amekuwa akitoa msaada kila mara, na sasa anaendelea na utamaduni huo, ili kuwapa faraja watoto hao pamoja na kutimiza ndoto zao kama watoto wengine.
 
“Msaada ambao nimetoa leo ni mchele Kilo 200, Sabuni ya unga kilo 30, unga wa sembe kilo 150, dagaa debe mbili, Maharage Kilo 40, mafuta ya kupikia ndoo moja, biskuti, vikombe 240, mifagio, stili waya, pamoja na mipira miwili ya michezo ya wasichana na wavulana,” amesema Mchungaji Kanunu.
 
Pia amewataka watoto hao wasome kwa bidii ili watimize ndoto zao, pamoja na kupendana wao kwa wao,ikiwamo na kuzingatia masharti ya wataalamu wa afya kwa kunawa mikono mara kwa mara ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko hasa kipindupindu na Corona. 
Naye mlezi msaidizi wa kituo hicho Loyce Daudi, amesema msaada huo wamepewa wakati muafaka, ambapo walikuwa na uhitaji nao, kutokana na baadhi ya wazazi wa watoto hao kuwatelekeza kituoni hapo na hakuna msaada wowote kutoka kwao.

 

 

 

Aidha amesema kitu hicho cha Buhangija Jumuishi, huwa kinalea watoto wenye ualbino, usikivu hafifu, na uoni, ambapo jumla yao wapo 213 na kipo chini ya Serikali, lakini baadhi ya mahitaji hayatolewi na Serikali na wanaishi kwa kutegemea wadau.
Nao baadhi ya watoto hao wenye mahitaji maalumu akiwamo Paschal Juma, wameshukuru kupewa msaada huo, na kutoa wito kwa wadau wengine waendelee kuwasaidia.
 
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mchungaji wa Kanisa la Baptist Nyanhende manispaa ya Shinyanga Renatus Kanunu, akizungumza kabla ya kutoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalumu ambao wanalelewa katika kituo cha Buhangija jumuishi.
Mchungaji Renatus Kanunu, akitoa nasaha kwa watoto wenye mahitaji maalumu ambao wanalelewa kwenye kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.
Mlezi msaidizi wa kituo cha kulea watoto wenye mahitaji maalumu cha Buhangija Loyce Daudi, akitoa shukrani ya msaada huo kwa niaba ya watoto hao wenye mahitaji Maalumu.
Mchungaji wa Kanisa la Baptist Nyanhende Manispaa ya Shinyanga Renatus Kanunu, akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto wenye mahitaji maalumu wanaolelewa kituo cha Buhangija , kikiwamo Chakula.
Mchungaji wa Kanisa la Baptist Renatus Kanunu, kushoto, akikabidhi msaada katika kituo cha kulea watoto wenye Mahitaji maalumu Buhangija.
Mchungaji wa Baptist Renatus Kanunu, kushoto, akikabidhi mipira miwili kwa ajili ya michezo kwa watoto hao wenye mahitaji maalumu katika kituo cha Buhangija.
Muonekano wa vifaa vilivyotolewa na mchungaji Kanunu
Mchungaji wa Kanisa la Baptist Nyanhende Manispaa ya Shinyanga Renatus Kanunu, akigawa Biskuti kwa watoto wenye mahitaji maalumu katika kituo cha Buhangija.
Watoto wenye mahitaji maalumu katika kituo cha Buhangija, wakiwa kwenye zoezi la kupewa msaada wa vitu mbalimbali na Mchungaji wa Kanisa la Baptist la Nyanhende Manispaa ya Shinyanga.
Watoto wenye mahitaji maalumu katika kituo cha Buhangija, wakiwa kwenye zoezi la kupewa msaada wa vitu mbalimbali na Mchungaji wa Kanisa la Baptist la Nyanhende Manispaa ya Shinyanga.
Watoto wenye mahitaji maalumu katika kituo cha Buhangija, wakiwa kwenye zoezi la kupewa msaada wa vitu mbalimbali na Mchungaji wa Kanisa la Baptist la Nyanhende Manispaa ya Shinyanga.
Na Marco Maduhu- Shinyanga.