Brass Band ya Magereza ikiowaongoza wahitimu wa Mafunzo kutoka Taaisisi ya Uongozi (Uongozi Institute) katika mahafali yaliyofanyika Mlimani City Dar es salaam jana.
…………………………………..
WAZIRI wa elimu na Mafunzo Profesa Joyce Ndarichako amewataka wahitimu wa Mafunzo kutoka Taaisisi ya Uongozi hapa nchini kwenda kuyatumia Mafunzo waliyoyapata vizuri ili kuleta chachu ya mafanikio katika sehemu zao za kazoi.
Amesema kuwa ni matumaini yake Mafunzo waliyoyapata wanakwenda kuimarisha dhana zima ya Uongozi kwenye sehemu zao za kazi na kuongeza uweledi katika kuchapa kazi.
Ndarichako ameyasema hayo wakati wa mahafari ya nne ya taasisi ya Uongozi Kwa ngazi mbalimbali Kwa watumishi wa umma na taasisi binafsi ambapo jumla ya wanafunzi 110 waliweza kuhitimu.
“Imani yangu nikwamba mmeiva na mmepikwa vizuri zaidi na mtatumia uwezo mliojengewa kuleta mabadiliko chanya kwenye nafasi zenu mnazofanyia kazi na mnaonekana wote mnadhamira kweli ya kuleta matokeo chanya.” Amesema Ndarichako
Nakuongeza kuwa ” mkayasimamie maeneo yenu ili kuleta mabadiliko chanya na kimsingi kabla ya kufanya Mafunzo mlifanya tathimini ili kuona maeneo ambayo wanataka kujengewa uwezo zaidi.”amesisitiza Profesa Ndarichako
Amefafanua kuwa matumaini yake wahitimu hao wanakwenda kuwa mfano zaidi na kwenda kuwa washauri wazuri zaidi kwenye maeneo yao hayo ya kazi hivyo wakajitazame na kuleta mabadiliko .
Pia amewataka wahitimu kwenda kuwafuza na wengine namna ya kusimamia wengine ili uwekezaji huo ukalipe nakwamba ili kuleta sifa za viongozi bora mahala pakazi ni mshikamano kutoruhusu migogoro kwenye maeneo yao ya kazi.
.”Hapa nataka kusema kuwa msiende kuwa vyanzo vya migogoro lakini mkawe chachu ya mafanikio kwani Mafunzo mliyopata yakaongeze malengo,chachu sehemu zenu za kazi .”amesema
Amesema Nchi ipo kwenye mpito kutokana na kuonfokewa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Magufuli na Kwa sasa taifa linajipanga upya chini ya Rais wa awamu ya sita Mh. Samia Hassan Suluhu.
“Niwakati wa kumuunga mkono Rais wetu Mh Samia Hassan Kwa kufanya kazi na kutoruhusu migogoro kwenye maeneo yenu na ninaimani kubwa mtakwenda kufanya vizuri.” Amesema Prefessa Ndarichako
Ndarichako ameongeza kuwa taaisisi hiyo ambayo imeazimisha miaka kumi tangu kuazisha kwako imekuwa ni taasisi ambayo inapika viongozi na kuwafanya kutumia Mafunzo wanayopata kuleta ufanisi kwenye kazi.
Licha Waziri Ndarichako pia mahafari hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ambapo pia katika mahafari hayo wengi wao walikuwa ni watumishi wa umma na binafsi.
Picha mbalimbali zikionesha wahitimu wakielekea ukumbini kwa ajili ya kutunukiwa vyeti vyao mara baada ya kuhitimu mafunzo ya uongozi.