Home Michezo YANGA YAICHAPA 3-1 GWAMBINA FC LIGI KUU TANZANIA BARA

YANGA YAICHAPA 3-1 GWAMBINA FC LIGI KUU TANZANIA BARA

0

TIMU ya Yanga SC leo imeibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Gwambina FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga SC yamefungwa na Ditram Nchimbi dakika ya 19, Bakari Mwamnyeto dakika 52 na Saido Ntibanzokiza dakika ya 90 na ushei, wakati la Gwambina limefungwa na Jimson Mwanuke dakika ya 49.
Kwa ushindi huo, Yanga SC imefikisha pointi 57 baada ya kucheza mechi 26 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tano zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao hata hivyo wana mechi nne mkononi.