Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bi. Neema Msita (kulia) akifafanua jambo kwa viongozi wa vyama vya Michezo kwa watu wenye ulemavu Wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Pauline Gekul na kushoto na kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya Olimpiki kwa watu wenye ulemavu, Bw. Tuma Dandi.
Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Pauline Gekul (kulia) akisisitiza jambo kwa viongozi wa vyama vya Michezo kwa watu wenye ulemavu Wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa vyama vya Michezo kwa watu wenye ulemavu wakimsikiliza Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Pauline Gekul (hayupo pichani) Wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kamati ya Olimpiki kwa watu wenye ulemavu, Bw. Tuma Dandi (kushoto) akitoa neno la shukrani kwa Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Pauline Gekul (katikati) mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa vyama vya Michezo kwa watu wenye ulemavu mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bi. Neema Msita.
Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Pauline Gekul (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa vyama vya Michezo kwa watu wenye ulemavu Wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Picha na WHUSM – Dar es Salaam