Balozi mdogo wa Burundi Mkoani Arusha, Leonidas Mbakenga akiongea na waandishi wa habari
…………………………………………………………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Balozi mdogo wa Burundi Mkoani Arusha, Leonidas Mbakenga amesema kuwa watamuenzi Hayati Rais Magufuli kwa namna ambavyo aliingoza Tanzania vizuri na kuweza kuleta maendeleo katika katika sekta mbalimbali.
Balozi Mbakenga aliyasema hayo wakati akisaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha ambapo alisema kuwa Hayati Rais Dkt Magufuli ameonyesha ushujaa mkubwa kwa namna ambavyo aliabzusha miradi mikubwa ambayo ilionekana haiwezekani lakini ikafanikiwa.
“Ameboresha mambo ya usafiri hata ikiwemo ndege, Reli na barabara ba sio faida kwa watanzania tu bali Afrika nzima hivyo waafrika tunaomboleza wote hakuna aliyetegemea kifo kama kifo chake kitatokea mapema kiasi hiki,” Alisema Balozi Mbakenga.
Alieleza kuwa Hayati Rais Dkt Magufuli alikuwa ni kiongozi ambaye lengo lake lilikuwa ni kuinua uchumi na kweli wanaona Tanzania imebadilika Kiuchumi, miundombinu na hata huduma za kijamii zimekuwa karibu na wananchi.
Aidha akimzungunzia Rais wa sasa wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu alisema kuwa ajipe moyo kwani hataweza kukamilisha mipango yote ya serikali walikuwa wanafanya pamoja ikiwemo kukamilisha miradi inayoendelea ili watanzania waendelee kuwa na matumaini ya kwamba huko mbele ni kuzuri.
Pia amewataka watanzania kuendelea kufikiri malengo aliyokuwa nayo Hayati Rais Dkt Magufuli ya kuhakikisha anavorwsha maisha ya yao huku wakimuunga mkono kwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii.