Home Uncategorized WAZIRI MKUU NA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR WAONGOZA MAELFU YA...

WAZIRI MKUU NA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR WAONGOZA MAELFU YA WANANCHI CHATO KUMUAGA HAYATI DKT.MAGUFULI

0

Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdulla pamoja na wananchi tayari wamefika katika Uwanja wa Magufuli uliopo Chato mkoani Geita tayari kwa ajili ya kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Msafara wa viongozi wanaosindikiza mwili wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ulipokuwa unaingia katika Uwanja wa Magufuli Chato mkoani Geita ili kuweza kuwapa nafasi wananchi wa Chato na maeneo ya jirani kutoa heshima zao za mwisho.

Wananchi wa Chato wakitoa heshima zao za mwisho kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.