Kiongozi wa Waislamu Madhehebu ya Shia Ithnasheriya Tanzania
Sheikh Hemed Jalala amemsifu aliyekuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt John Magufuli kwa ujasiri wake mkubwa na wa wazi wa kumbambana dhidi ya Mabeberu
ambao walikokuwa wanainyonya nchi yetu.
“Hayati Dkt John Magufuli alitueleza jambo kumbwa mno na jambo
muhimu kuwa kutambua na kutueleza mbinu za mabeberu, mbinu za wanyonya damu,
watu wanaotaka siku zote wa ishi kwa migongo ya wa Tanzania na migongo ya wa
Afrika.Kwa kweli kwa tendo lake la kuuzungumza ubeberu na kuwazungumza wanyonya
damu, na kwamba lau si wanyonya damu, wa Afrika tusinge ishi katika mazingira
ya umasikini na hali tuliyonayo na wala tusinge kuwa na maradhi haya tuliyo
nayo yanayotumaliza kila siku” alisema Kiongozi Sheikh Jalala
Kiongozi Sheikh Jalala alisema hayo jana, katika Khutba Swala
ya Ijumaa, Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es Salaam na kusema kuwa Hayati Dkt
John Magufuli atakunbukwa kwa jambo lake la kumtanguliza Mungu kwa kila jambo
na kila hali.
“Hayati Dkt John Magufuli alimtanguliza Mungu katika mambo
yake yote, katika hotuba zake, katika mikutano yake, awe amekaa awe amesimama,
kwa kweli Mungu alimtanguliza mbele. Bali wakati mwingine huwenda Viongozi wa
Dini walirudi nyuma, yeye alikuwa mstari wa mbele katika kumuamini Mungu”.
Alisema Kiongozi Sheikh Jalala.
Aidha Kiongozi Sheikh Jalala amesema kuwa Hayat Dkt John
Magufuli hatosahauliwa katika Nyanja ya kudumisha na kuenzi Amani, Upendo,
mshikamano na Umoja na kuwataka Watanzania wasikubali kuhatarisha Amani,
mshikamano na umoja.
Hayati Dkt. John Pombe Magufuli enzi za uhai wake. |
“Hayati Dkt John Magufuli alikuwa mpenda Amani, mpenda umoja,
mpenda mshikamano ambayo ndio misingi mikubwa ya Taifa letu la Tanzania. Taifa
la Tanzania litapigiwa mifano, na wenzetu wanaona gere, utulivu tulionao, Amani
tulionayo na mshikamano tulionao” Alisema Kiongozi Sheikh Jalala.
“Niwaombe Watanzania kwenye kipindi hiki ambacho ni cha
majonzi, ni kipindi cha huzuni, ni kipindi cha kutafakari, tuzidi kudumisha
Umoja, mshikamano wetu, tuzidi kuenzi Amani ya nchi yetu na tusiyakubali maneno
ya mtu yeyote yanayoandikwa iwe katika facebook, iwe ni twitter, iwe ni
Instagram, iwe ni mahala gani, ambapo maneno hayo yatajaribu kuwatikisa
Watanzania na kuwatoa katika mstari wao wa umoja, amani na mshikamano, Poleni
sana Watanzania, Pole sana Mama yetu Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu” Alisema Kiongozi Sheikh Jalala.