Home Mchanganyiko WACHIMBA MADINI WAMLILIA HAYATI MAGUFULI,WAMPONGEZA PIA SAMIA

WACHIMBA MADINI WAMLILIA HAYATI MAGUFULI,WAMPONGEZA PIA SAMIA

0
********************************
Na Woinde Shizza ,  ARUSHA
Mwenyekiti wa taifa wa chama cha wafayabiashara wa madini Tanzania Sammy Mollel ameeleza kuwa wamepokea kwa masikitiko makubwa na simanzi taarifa za kifo cha hayati Rais Dkt John Magufuli kwani alikuwa jemedari wao katika kusimamia biashara ya madini. 
Mollel aliyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo alisema kuwa hawakuamini walipopata taarifa za awali lakini baada ya makamu wa Rais mama Samia Suluhu kutangaza ndipo wakagundua kuwa ni kweli.
“Kifo cha hayati Rais Dkt Magufuli kimetugusa sana wafanyabiashara wa madini jitihada na maono yake yalipandisha makusanyo ya tozo za madini kutoka millioni 160 kwa mwaka hadi kufikia billioni 2,”Alisema Mollel. 
Alisema wameona juhudi zake binafsi za kujengwa ukuta Mererani ambapo mpaka sasa wameona faida kubwa sana za ukuta huo ikiwemo kulinda usalama wao wanapokuwa katika kazi zao tofauti ma awali, uzalishaji kuongezeka pamoja tozo za serikali kukusaywa kwa kiasi kikubwa. 
“Ameifanikisha sana sekta  ya madini kwa kuelekeza masoko ya madini yajengwe kila mkoa wenye shughuli za uchimbaji madini, tulimweleza kero zetu kuhisiana tozo sumbufu, alizipokea na kutoa maelekezo kwa Bunge kurekebisha ambayo ilikuwa ni tozo ya ongezeko la thamani, VAT na tozo ya zuio na kushuka kutoka asilimia 18 hadi kufikia asilimia 5,” Alieleza. 
Alifafanua kuwa walimpenda sana lakini Mungu alimpenda zaidi na kama Tamida wanawasihi watanzania kuwa na subira kipindi hiki cha maombolezo na kuyaezi yale yote aliyowaachia kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kuigia katika uchumi wa juu. 
“Kwa sababu yake leo Tanzania tuna heshima kubwa sana duniani kwa kuingia uchumi wa kati na uchumi wa viwanda na sisi tunaahidi  tutamuenzi kwa kuongeza dhamani ya madini na kufika mbali zaidi kama alivyotuazishia,”Alieleza.
 Kwa upande wake bilionea wa madini  aina ya ruby kutoka wilayani Longido   Gabriel Sendeu Laizer alisema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa  sana taarifa za kifo cha Rais Magufuli kwani alikuwa  akiwathamini wachimbaji wadogo wa madini haswa wazawa wa kitanzania.
Alisema kuwa Rais Magufuli  aliweza kuwapa haki zote za uchimbaji wa madini pamoja na umiliki wa madini kwa kuwawezesha pamoja na kuwa na nguvu zao wenyewe ambapo pia hakujali kwamba wachimbaji wazawa  wataweza kuchimba au awawezi kuchimba .
Alisema kuwa kutokana na Magufuli  kuwathamini  na kuwapa fursa watanzania wameweza kuchimba madini na kujipatia kipato.
“Amewezesha migodi ambayo ilikuwa imesimama kutokana na kuachwa na wazungu  kuchukuwa  na wazawa , kazi zinaendelea na ndio  maana unaona hata  mapato  yanayotokana na madini  yameongezeka kuliko wakati mungine wowote ule” alisema Sendeu.
Alimpongeza  Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuteuliwa kuongoza nchi ya  Tanzania  ,na kukwambia kuwa wanamtakia mafanikio mema katika kazi zake za kuletea nchi maendeleo 
Alisema kuwa wanaamini kabisa Rais ata endeleza yale yote mema ambayo   hayati Magufuli  ameyafanya ,ikiwemo miradi mbalimbali waliyoiacha .
415 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa  wa Arusha Ndugu Zelothe Stephen Zelothe akisaini kitabu cha Maombolezo ya Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika Jengo la Ccm Mkoa mapema hii leo.
Bilionea wa madini aina ya Ruby kutoka Kijiji Cha Mundarara Wilayani Longido mkoani Arusha Gabriel Sendeu Laizer akisaini kitabu Cha maombolezo jana ya aliekuwa Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hayati John Magufuli kilichopo Katika viwanja vya ofisi za mkuu wa mkoa wa Arusha (picha na Woinde Shizza , ARUSHA).