Home Mchanganyiko Wadau mbalimbali mkoani Arusha wamlilia Hayati Rais  Magufuli .

Wadau mbalimbali mkoani Arusha wamlilia Hayati Rais  Magufuli .

0
Mmoja wa wafanyabiashara mkoani Arusha , Naushad Hussein akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na kifo Cha Hayati Dokta Magufuli (Happy Lazaro).
******************************************
Happy Lazaro,Arusha 
Arusha.Wafanyabiashara mbalimbali mkoani Arusha wamemlilia Hayati Rais John Pombe Magufuli kwa namna ambavyo aliweka nidhamu kwenye biashara na kuendelea kuwapa moyo wafanyabiashara mbalimbali kuchangia Kodi kutokana na utendaji kazi mzuri aliokuwa nayo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wafanyabiashara hao, Mkurugenzi wa makampuni ya Benson yaliyopo mkoani Arusha Naushad Hussein amesema kuwa,kifo Cha Rais Magufuli ni pigo kubwa kwa nchi yetu kutokana na jinsi alivyoitengeneza nchi kwa kipindi cha miaka mitano tu.
Naushad amesema kuwa,Hayati Rais Magufuli aliweza kuweka nidhamu kwenye biashara hali iliyochangia kuongezeka kwa mapato serikalini kupitia kodi na hatimaye kuweza kutekelezwa kwa miradi mbalimbali ya maendeleo,kwani hapo zamani kulikuwa hakuna nidhamu katika ulipaji Kodi tofauti na Sasa hivi.
“Kwa kweli Rais Magufuli alituwekea mazingira mazuri Sana ya kulipa kodi kutokana na kuwa tulikuwa tunaona kazi zake kupitia kodi tunazotoa ,hivyo unaona hata ukichangia kodi kuna miradi inayofanyika ,hivyo Rais Magufuli aliweza kuchangia maendeleo kwa kiasi kikubwa Sana hasa kwenye maswala ya uchumi.”amesema .
Amefafanua kuwa, Hayati Rais Magufuli aliweza kuwaondolea hofu wananchi kuhusu ugonjwa wa COVID 19 na kuwataka kuomba Mungu badala ya kuwekwa “lockdown”kwani wananchi wangewekwa lockdown wangepata shida Sana ikilinganishwa maisha yetu ni ya kujitafutia kila siku.
Naye  Meneja wa Tanroad mkoani Arusha,Injinia John Kalupale amesema kuwa,kwa kweli nchi imepata pigo kubwa sana na ni msib wa kitaifa ambao hauzoeleki kwani alikuwa mtu ambaye hakubagua mtu yeyote dini au kabila alitenda haki kwa watanzania wote .
Hata hivyo amewaasa watanzania kuwa ,huu sio muda wa kunyoosheana vidole kwani yapo mengi mazuri ambayo ameyafanya  tusonge mbele kama Rais wetu na tuwe na umoja bila  kuwa na upendeleo wowote kwa maslahi ya nchi yetu.
Naye Meya wa jiji la Arusha , Maximilian Iraghe amesema kuwa,watamkumbuka Rais Magufuli kwa uzalendo wake mkubwa aliokuwa nao wa kupenda nchi yake , hivyo msiba huo wameupokea kwa masikitiko makubwa Sana .
“kwa kweli wananchi wa Arusha tutamkumbuka Sana kwa mengi aliyoyafanya kwani Taifa kwa ujumla limepoteza mtu ambaye angetuvusha kwenye changamoto mbalimbali ,tunaomba Mungu  mama Samia aweze kuvaa viatu vya Hayati Magufuli.”amesema.