Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa akifanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya Bw. Manfredo Fanti leo Machi 17, 2021 Jijini Dar es Salaam ambapo amemweleza maombi ya Ushirikiano na nchi za Ulaya katika masuala ya ‘resale right’ katika kazi za Sanaa ya ufundi.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa (wasaba kulia) akiwa katika picha ya pamoja na na Balozi wa Umoja wa Ulaya Bw. Manfredo Fanti (watano kushoto) leo Machi 17, 2021 Jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya mazungumzo yaliyolenga mashirikiano katika sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Wakurugenzi wa kiseka wa Wizarani na Wakuu wa Taasisi zilizochini ya Wizara hiyo, wa pili kuchoto ni Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimliki Tanzania (COSOTA) Bibi. Doreen Sinare.
Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimliki Tanzania (COSOTA) Bibi. Doreen Sinare akitoa pongezi na shukrani kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa (hayupo pichani) kwa kusemea suala la ‘resale right’ kwa Balozi wa Umoja wa Ulaya Bw. Manfredo Fanti wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika leo Machi 17, 2021 Jijini Dar es Salaam mbele ya Wakurugenzi wa Idara wa Wizarani na Wakuu wa Taasisi zilizochini ya wizara hiyo.
………………………………………………………………………………………….
Anitha Jonas – COSOTA , Dar es Salaam
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa leo Machi 17,2021 amefanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya Tanzania na Afrika Mashariki Mhe. Manfredo Fanti aambapo amemwomba ushirikiano katika nchi za Ulaya katika kazi za Sanaa ya Ufundi za Wasanii wa nchini kunufaika na mauzo ya kazi zao zinapouzwa katika nchini hizo kupitia minada mikubwa kwa kulingana na Kanuni ya ‘resale right’ inayosimamiwa na Taasisi ya Hakimiliki na Hakishiriki Tanzania (COSOTA).
Akiendelea na mazungumzo hayo Waziri Bashushwa alimweleza balozi huyo kuwepo kwa changamoto kwa Sanaa ya Tingatinga nchini ya kurubuniwa katika mikataba mbalimbali mauzo yake ya saana yake ambapo imeleta changamoto ya suala la Hakimiliki, ambapo changamoto hiya mikataba hiyo inafanyiwa kazi na COSOTA hivi sasa.
Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho Mhe.Bashungwa aliezea Taasisi ya Hakimiliki Tanzania chini ya Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Bibi. Doreen Sinare imekuwa ikilifuatulia suala hilo, kufuatia mikataba mibovu waliyoingia na kampuni mbalimbali..
‘Ushirikiano huu utaleta chachu katika utatuzi wa uhitaji wa masoko ya uhakika kwa kazi za Sanaa ya Ufundi na kuchangia kukua kwa Sanaa hii ambayo wasanii wataifa hili wanaifanya vizuri ,’alisema Mhe.Bahungwa.
Aidha, Waziri Bashungwa alieleza juu ya mashirikiano na COSOTA, jitihada za serikali katika kuimarisha taasisi hiyo iliiweze kufanya majukumu yake vyema hususan katika kulinda kazi za Sanaa hasa muziki na kuongeza kipato kwa wasanii na Wabunifu sababu ni moja ya taasisi yenye tija na maslahi mapana ya taifa na yenye dhamana ya kulinda hakimili nchini.
Katika mazunguzo hayo Waziri huyo amesisitiza mashirikiano katika Taasisi za COSOTA, TASUBA na Chuo cha Malya. Mazungumzo hayo kati ya Balozi huyo na Waziri yalifanyika mbele ya Wakuu wa Taasisi zilizochini ya wizara hiyo kwa lengo la kila mmoja kueleza maeneo ya taasisi yake ambayo angependa kushirikiana na ubalozi huo.
Kwa upande wa Balozi wa huyo wa Umoja wa Ulaya nchini Bw.Manfredo Fanti alieleza dhamira yake ya kutoaushirikia katika sekta hizo kwa kuomba baadhi ya watendaji wake kukutana na viongozi hao wanaosimamia sekta ya habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo kwa lengo la kujipanga vyema namna wanavyoweza kufanya kazi katika maeneo yao.
MWISHO