Msajili Mkuu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Wilbert Chuma akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za mahakama hiyo leo Jijini Dar es Salaam
PICHA NA EMMANUEL MBATILO
********************************
Mahakama kuu ya Tanzania imejipanga kuweka utaratibu bora wa kusikiliza mashauri yote ili kuondoa mrundikano wa mashauri katika mahakama mbalimbali nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Msajili Mkuu wa Mahakama kuu Tanzania Wilbert Chuma wakati akizungumza na waandishi wa habari akitolea ufafanuzi wa masuala ya kimahakama pamoja taarifa iliyokuwa imeandikwa kwenye gazeti la Jamhuri la Machi 9-15 mwaka huu.
Msajili huyo amesema kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamekuwa wakifanya juhudi za kuhakikisha linakabiliana na mrundikano wa mashauri ambapo ameeleza kuanzia mwezi Januari mpaka Machi mwaka huu mashauri 2814 .
Kwa upande wake Mkurugenzi wa usimamizi wa Mashauri Mahakama ya Tanzania Desdery Kamugisha ametolea ufafanuzi kwa Jamhuri kutoa mashauri na kuyarejesha tena mahakamani.
Kevin Muhina ni Msajili wa Mahakama ya Rufani ameeleza utekelezaji wa kuanza kutumia lugha ya Kiswahili kwamba wanaendelea na mchakato huo ili kufanya wananchi wawe na uelewa wa sheria.
Katika hatua nyingine Msajili Mkuu wa Mahakama Kuu Tanzania Wilbert amesema ndani ya mahakama hakuna sera ya kuchelewesha kesi bila sababu lakini pia hakuna Wakili au Jaji anayependa kuchelewesha shauri au kumuweka mtuhumiwa mahabusu bila ya sababu kama ilivyochapishwa katika gazeti hilo.