Home Mchanganyiko RUWASA PWANI KUWAONDOLEA KERO YA UPATIKANAJI WA MAJI SAFI WANANCHI WA KATA...

RUWASA PWANI KUWAONDOLEA KERO YA UPATIKANAJI WA MAJI SAFI WANANCHI WA KATA YA MAKURUNGE BAGAMOYO

0

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mh. Zainabu Kawawa wa kushoto wakiwa anatazama juu ya mnara  kuangalia tanki kubwa la maji halipo pichani  linalojengwa katika kitongoji cha Mtoni lenye ujazo wa lita zipatazo elfu 50 wakati alipokuwa mgeni rasmi katika uwekaji wa jiwe la msingi la mradi huo, kulia kwake ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Pwani  Injinia Beatrice Kazimbazi.

Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Bagamoyo Injinia James Kionaumela wa kwanza akiwa katika msafara wa miguu akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa wa pili yake pamoja na viongozi wengine wa Ruwasa pamojana na halmashauri kwa ajili ya kwenda kujionea utekelezaji wa miradi ya maji mbali mbali pamoja na mitaro inayochimbwa ili kutandaza mabomba.

Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Pwani  Injinia Beatrice Kazimbazi akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo hayupo pichani kuhusina na utekelezaji wa miradi mbali mbali ambayo inafanywa na Ruwasa katika maeneo mbali mbali ya Wilaya hiyo.

 Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa wa kulia akipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Bagamoyo Injinia James Kionaumela baada ya kukamiliza zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa maji wa kitongoji cha Mtoni.

i Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo wa kulia Zainabu Kawawa akiwa anaangalia ujenzi wa mtaro ambao umechimbwa maalumu kwa ajili ya utekelezaji wa ulazaji wa mabomba kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo ambao utawanufaisha wananchi  mbali mbali.

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo Mohamed Usinga akizungumza kuhusiana na jinsi mradi huo ambao umetekelezwa na Ruwasa utakavyowasaidia na kuwaondolea kero na changamoto ya wananchi kutembea umbari mrefu.

Muonekano wa Kibao ambacho kiliandaliwa maalumu kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi huo  wa maji katika kitongoji cha Mtoni kata ya Makurunge ambapo sherehe za uwekaji wa jiwe hilo limefanywa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)

…………………………………………………………………………………………….

NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO

WANANCHI  zaidi ya 1169 ambao wanaishi katika  kitongoji cha mtoni kilichopo katika kata ya Makurunge Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani ambao walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya kutembea umbari mrefu kwa ajili ya kutafuta maji safi na salama hatimaye wanatarajia kuondokana na adha hiyo baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji safu na salama  ifikapo machi 30 mwaka huu ambao unatekelezwa na Ruwasa.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa wakala wa maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA)  Wilaya ya Bagamoyo Injinia James Kionaumela wakati akitoa taarifa  kwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe zilizoandaliwa  maalumu kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi wa mradi huo ambao utakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa kata hiyo.

Sherehe za uwekaji wa jiwe hilo la msingi ni moja kati ya shughuli mbali mbali ambazo zinatekelezwa na Ruwasa ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji duniani lengo ikiwa ni kuwasogezea huduma wananchi kuondokana na kero ya kusumbuka usiku na mchana kwa ajili ya kutafuta maji safi na salama katika maeno ya mbali na kuweka mipango endelevu ambayo itasaidia katika kuboresha sekta ya maji hasa katika maeneo ya vijijini.

Aidha Meneja huyo alifafanua kwamba katika mradi huo unatekelezwa kupitia mfuko wa maji kupitia fedha za mfuko wa maji wa NWF mbapo chanzo chake cha maji kinatokea katika maeneo ya Chalinze kutoka kwenye mradi wa maji Dawasa.

Pia aliongeza kuwa mradi huo unatekelezwa kutimia wataalamu wa nadni ambapo kazi zilizofanyika na kufanyiwa utekelezaji ni kujenga tanki kubwa la maji ambalo lina litakuwa na ujazo wa lita zipatazo 50,000 ambalo limejengwa juu ya mnara wenye mita zipatazo 12 na kwamba ununuzi na ulazaji wa bomba zenye vipenyo mbali mbali wa kilometa 5.25  ambapo pia kutakuwa vituo nane kwa ajili ya wananchi kutekea maji.

Kwa upande wake MKUU wa Wilaya ya Bgamoyo Zainabu Kawawa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika wakati  sherehe  hizo za  uwekaji wa jiwe la msingi alitoa pongezi wa viongozi wa Ruwasa kwa kuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kujikita zaidi katika kuwaondolea adha wananchi katika suala zima la upatikanaji wa maji safi na salama.

“Kwa kweli mimi kama Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Ruwasa kwa juhudi zao wanazozifanya na kunialika katika kuweka jiwe l msingi katika mradi huu wa maji nina hakika kabisa utaweza kuwa ni mkombozi mkubwa katika kuwakomboa wananchi  hasa wakinamama ambao wamekuwa wakipata shida ya kutembea umbari mrefu kwa hivyo mradi huu kwetu ni mkombozi mkubwa,”alisema Kawawa.

Pia Kawawa alisema kwamba lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inaweka mikakati madhubuuti kwa ajili ya kuwaondolea changamoto mbali mbali ya upatikanaji wa maji safi na salama na kuhakikisha kuwa inamtua mama ndoo kichwani pamoja na kuimarisha miundombinu ya mabomba ambayo yanatumika katika miradi hiyo.

Kawawa alifafanua kwamba katika eneo hilo la ujenzi wa mradi wa maji alishafika mara kwa mara na kuzungumza na wananchi wa kitongoji hicho cha mtoni hivyo amewaomba kuwa walinzi wazuri wa kuutunza mradi huo ambao utaweza kusawasaidia kwa kiwango kikubwa na kuondokana na ile hali ya kusaka maji kwa kutembea umbari mrefu.

Meneja wa wakala wa maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) Mkoa wa Pwani Injinia Beatrice  Kazimbazi alifafanua kwamba katika halmashauri ya Bagamoyo wameshatekeleza miradi ya maji zaidi ya tisa ikiwa pamoja na kufanya ukarabati wa miundombinu ya mabomba ili kuweza kuwafikishia huduma  ya maji safi na salama wananchi.

“Katika Wilaya ya Bagamoyo tangu kunzishwa kwa Ruwasa tunatekeleza miradi mbali mbali ya maji na lengo letu kubwa ni kuhakikisha kwamba tunawaondolea changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama wananchi wetu na  kwamba gharama za fedha ambazo zimetumika katika mradi wa kitongoji cha mtoni ni  zaidi ya shilingi milioni 181  na kwamba bado kuna miradi mingine inaendelea kujengwa  katika Wilaya ya Bagamoyo.,”alisema Injinia Beatrice.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo Mohamed Usinga pamoja na Mwenyekiti wa kamati ya maji Abdul Pyalla walisema kwamba kukamilika kwa mradi huo wa maji kambao unajengwa katika kitongoji cha mtoni utaweza kuwasaidia wananchi mbali mbali wa maeneo hayo pamoja na mengine ya jirani kuondokana na kero kubwa ambayo walikuwa wanaipata kwa kipindi kirefu.

“Kwa kweli Uongozi wa Ruwasa hasa meneja wetu wa Wilaya pamoja na Meneja wetu wa Mkoa Injinia Beatrice kwa kuwa wanachapa kazi kwa maeneo yetu ya bagamoyo hasa katika maeneo ya vijijini wametutendea haki maana hii changamoto ya maji katika baadhi ya maeno ilikuwepo lakini kutokana na juhudi zao kwa kweli sisi kama madiwani hili jambo kwetu ni kubwa sana maana itakapofika machi 30 mwaka huu wananchi wetu wataondiokana  kabisa na shida ya maji,”walisema madiwani hao.

MAADHIMISHO ya wiki ya maji kwa mwaka huu kauli mbiu yake inasema kwamba thamani ya maji ni Uhai na maendeleo.