Home Mchanganyiko Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa amezungumza na ubalozi...

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa amezungumza na ubalozi wa Qatar kusaidia sekta ya  Sanaa na Michezo nchini .

0

****************************************

Waziri Bashungwa ameongoza mazungumzo hayo machi 17 jijini Dar es Salaam  akiwa na Wakuu wa Taasisi zilizochini ya wizara hiyo walipo kutana na Balozi wa Qatar nchini Tanzania Mhe. Hussain Ahmad Al – Homaid.

 Kikao hicho kilikua na lengo la kuona  namna Qatar itakavyoweza kusaidia tasnia ya Filamu nchini, Masoko kwa Sanaa za Ufundi, uendelezaji wa viwanja vya michezo pamoja na kubadilishana uzoefu katika sekta ya Habari.

“Kutokana na Ilani ya Chama chetu Tawala CCM tuna nia yakuongeza sana ajira kwa vijana na vijana wengi wapo katika sanaa na michezo, naomba ikiwezekana kupata  library ya vifaa vya kutengenezea  Filamu kutokana na kuwa na uhaba wa vifaa vya kisasa na wasanii wengi vijana hawa mudu gharama ya vifaa hivyo hivyo”alisema  Mhe. Waziri Bashungwa.

Pia Mhe.Waziri Bashungwa ameomba ubalozi huo kuisaidia timu ya Taifa   katika maandalizi yake ya michuano ya kushiriki kombe la Dunia ambapo timu hiyo ina mechi tatu  wanazotarajia kucheza ili  kufuzu kucheza kombe hilo.

 Aidha Mhe. Bashungwa ameomba  ushirikiano na Qatar katika kujenga  Maktaba ya vifaa vya kuzalisha filamu ambayo  Serikali imedhamiria kuijenga kwa lengo la kukuza tasnia hiyo na kuongeza ubora kwa kazi za filamu zinazozalishwa nchini.

Kwa upande wake, Balozi wa Qatar  ameahidi kushirikiana  na Serikali ili timu ya Taifa iweze kupata  nafasi  kushiriki katika kombe la Dunia  linaloandaliwa na nchi hiyo  mwaka 2022.

Vilevile Mkuu wa Taasisi ya Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbet Makoye ameomba ubalozi huo kushirikiana na Taasisi hiyo katika  kubadilishana washiriki katika Tamasha la kimataifa la Bagamoyo international festival na Qatar Art Festival ili kujijengea ujuzi zaidi katika tamaduni na sanaa za nchi zote mbili.